Featured Kitaifa

KAMPENI YA BADILI TABIA SEPESHA RUSHWA YAZINDULIWA DODOMA,RC MTAKA ATOA NENO

Written by mzalendoeditor

MABALOZI wa Kampeni ya badili tabia sepesha rushwa (ACVF) wakiwa katika Maandamano ya Amani ya uzinduzi wa Kampeni kutoka Nyerere Square mpaka Kilimani Club jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza na Mabalozi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya badili tabia sepesha rushwa (ACVF) iliyofanyika jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya badili tabia sepesha rushwa (ACVF) iliyofanyika jijini Dodoma.

Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Victor Swella,akielezea jinsi Ofisi hiyo itakavyoshirikiana na ACVF kutoa elimu kwenye makundi mbalimbali kwenye mapambano ya Rushwa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya badili tabia sepesha rushwa (ACVF) uliofanyika jijini Dodoma.

Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Victor Swella,akifafanua jambo kwa mabalozi wa kupiga rushwa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya badili tabia sepesha rushwa (ACVF) uliofanyika jijini Dodoma.

MLEZI wa Sauti ya Wapinga Rushwa (ACVF) Bw.Abell Otieno,akitoa salamu za Taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya badili tabia sepesha rushwa (ACVF) uliofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mtendaji wa  Mabolozi wa Sauti ya wapinga rushwa (ACVF) Kubega Dominiko,akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Sauti ya wapinga Rushwa (ACVF) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya badili tabia sepesha rushwa (ACVF) uliofanyika jijini Dodoma.

SEHEMU ya Mabalozi wa Kupiga Rushwa (ACVF) wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya badili tabia sepesha rushwa (ACVF) iliyofanyika jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akikata utepe kuashiria rasmi uzinduzi wa Kampeni ya badili tabia sepesha rushwa (ACVF) uliofanyika jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akikabidhiwa vitendea kazi na Katibu Mtendaji wa  Mabolozi wa Sauti ya wapinga rushwa (ACVF) Kubega Dominiko mara baada ya kuzindua Kampeni ya badili tabia sepesha rushwa (ACVF) iliyofanyika jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akigawa Vyeti kwa Mabalozi waliohitimu Mafunzo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya badili tabia sepesha rushwa (ACVF) iliyofanyika jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi mara baada ya kuzindua Kampeni ya badili tabia sepesha rushwa (ACVF) iliyofanyika jijini Dodoma.

……………………………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka, amezindua Kampeni ya badili tabia sepesha rushwa (ACVF) itakayo tekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam na Arusha kwa lengo la kusaidia harakati za kuzuia vitendo vya rushwa nchini.

Akizungumza wakati wa  uzinduzi huo jijini Dodoma Mtaka,ameitaka Taasisi ya Sauti za wapinga rushwa (ACVF) kufanya kazi kwa malengo yaliyokusudiwa ili kukomesha vitendo vya rushwa nchini.

Kampeni hiyo inahusisha mabolozi 365 ambao wamepatiwa mafunzo na Tasisi ya kupinga na kupamba na rushwa nchini TAKUKURU.

Mtaka amewahakikishia mabalozi wa kupinga rushwa kuwa atawapa ushirikiano ili kuhakikisha wanafanikisha kampeni hiyo.

“Nimefurahi mno kuona kuna watu bado hawalali wanaendeleza mapambano ya rushwa,nani asiyependa kuona rushwa inatokomezwa niwaahidi kwa nafasi yangu nitafanya mkutano mkubwa na kuwashirikisha Klabu zote za wapinga rushwa wote wa shule ya msingi hadi vyuoni hii itasaidia kutengeneza mabalozi wa rushwa kwa kila maeneo ambao serikali imepeleka fedha za miradi,”amesema Mtaka

Hata hivyo Mtaka amesema kuwa pamoja na juhudi hizo serikali kuona kunakuwa na mabalozi wapinga rushwa hadi vyuoni ambapo wanafunzi wengi wanalalamika kwamba mambo hayako sawa kutokana na rushwa ya ngono.

“Tunaposepesha rushwa lazima tuone umuhimu wa kuingia kiundani zaidi ili tusepeshe kiukweli tusipoongeza juhudi hata watoto wetu wanaofanyiwa ukatili wa kingono mashuleni wakija kuajiriwa nao wanaweza kurithi vitendo hivyo”ameeleza

Kwa upande wake Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma Victor Swella amesema kuwa Ofisi hiyo itashirikiana na ACVF kutoa elimu kwenye makundi mbalimbali kwenye mapambano ya Rushwa.

“Tupeleke zaidi elimu kwa watu wa chini ambao wananyimwa haki yao kwa sababu ya rushwa kuna wengine hata hawajui viashiria vya rushwa ni kazi yetu kuwaelimisha bila kuchoka ili kila mtu aishi kwa amani na utulivu ,”amesema

Awali Katibu Mtendaji wa  Mabolozi wa Sauti ya wapinga rushwa (ACVF) Kubega Dominiko amesema kuwa Kampeni ya Badili tabia Sepesha Rushwa ilizinduliwa Mei 1, 2022,  jijini Dar es Salaam chini ya afisa wa dawati la elimu kwa umma TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni.

Hata hivyo, amesema kuwa baada ya kuzinduliwa jijini Dodoma pia hivi karibuni itazinduliwa Jijini Mwanza na kukamilisha mikoa yote mitatu.

Kubega amesema kuwa ACVF ni Taasisi inayolenga kuongeza ufahamu juu ya Rushwa ngazi ya Kitaifa,wao ni asasi pekee iliyoamua kupaza sauti na kuendeleza harakati za Kupambana na kuzuia rushwa nchini Kwa kauli Moja ya BADILI TABIA #SEPESHARUSHWA

Amesema kuwa Kampeni  hii ya Badili tabia #SepeshaRushwa inaendeshwa na Watanzania Wazalendo ambao kiu Yao kubwa ni Kupambana na adui mbaya Rushwa ambao Kwa ujumla wao Ndio huitwa MABALOZI WA SAUTI ZA WAPINGA RUSHWA.

”Baada ya Uzinduzi Wa Kampeni hii hapa Jijini Dodoma Taasisi itatangaza usajili Rasmi Wa awamu ya pili na kuendesha Mafunzo ambayo kilele chake kitaazimishwa Jijini Arusha ili kufikia Malengo tuliyojiwekea. Arusha wakae Mkao Wa Kula.”amesema Bw.Kubega

About the author

mzalendoeditor