Featured Michezo

YANGA YAITEKA DAR ES SALAAM,MAPOKEZI YAKE YAWEKA REKODI BARABARA ZAFUNGWA

Written by mzalendoeditor

MABINGWA wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara timu ya Yanga imelisimamisha Jiji la Dar es Salaam wakati wakizunguka na Kombe lao wakiwa kwenye gari la aina yake.

Pia wakapita njia ya  Kariakoo nako wakasimamisha shughuli zote  hakuna anayepita wala anayefanya manunuzi.

Msafara wa Yanga umetinga Kariakoo karibu kabisa na makao makuu ya watani wa jadi Simba kisha mashabiki wao kusimamisha wakiwaringia wenzao.
Mwisho Yanga wakamalizia kwa kuanza kuimba kwa kishindo wakitaja jina la wadhamini wao GSM GSM GSM GSM na kuwanyamazisha wenzao.

About the author

mzalendoeditor