Featured Kitaifa

WAZIRI JAFO: BAJETI IMEZINGATIA HIFADHI YA MAZINGIRA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani jafo amesema Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2022/22 iliyowasilishwa hivi karibuni imezingatia masuala ya mazingira.

Amesema ipo miradi mbalimbali ya kimazingira iliyoanishwa ambayo imeanza kutekelezwa ambayo itasaidia kupunguza hewa ya ukaa.

Amesema hayo leo Juni 24, 2022 wakati akichangia mjadala wa Bajeti Kuu bungeni jijini Dodoma.

Waziri Jafo alifafanua kwa kusema kuwaTanzania imejipanga kupunguza kiwango cha hewa ya ukaa kwa asilimia 30 hadi 35 kupitia miradi mbalimbali.

Alibainisha kuwa bajeti hiyo imekuja na vipaumbele ambavyo vitasaidia katika masuala ya hifadhi na utunzaji wa mazingira.

Alisema kuwa Mradi wa treli ya Kisasa (SGR), Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere litasaidia kupunguza ukataji wa miti ovyo, Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (DART) unasaidia kupunguza msongamano na hivyo kupunguza hewa ya ukaa.

Aidha, waziri ni halmshauri chache zinafaidika na baishara ya hewa ya ukaa ikwemo ya Tanganyika mkoani Katavi hivyo kutokana na hilo Serika imeanza kuandaa Mwongozo wa Kitaifa wa Biashara ya Hewa Ukaa utakaotumiwa na wawekezaji, taasisi na watu binafsi wenye nia kufanya biashara hii hapa nchini.

Dkt. Jafo aliongeza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na wadau itakuja na kanuni za namna ya utekelezaji wa mwongozo huo ili nchi ifaidike na biashara ya hewa ya ukaa na hata kuchangia katika bajeti.

 

About the author

mzalendoeditor