Featured Kitaifa

SERIKALI YATANGAZA BEI UKOMO ZA HUDUMA YA MAJI

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Maji Mhe.Jumaa Aweso,akizungumza wakati katika hafla ya kukabidhi taarifa ya utendaji ya wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) kwa mwaka 2020/2021 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Maji.Mhandisi Maryprisca Mahundi,akizungumza  wakati wa hafla ya kukabidhi taarifa ya utendaji ya wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) kwa mwaka 2020/2021 jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde ,akizungumza  wakati wa hafla ya kukabidhi taarifa ya utendaji ya wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) kwa mwaka 2020/2021 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) Prof. Idrisa Mshoro,akizungumza  wakati wa hafla ya kukabidhi taarifa ya utendaji ya wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) kwa mwaka 2020/2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clement Kivegalo,akizungumza  wakati wa hafla ya kukabidhi taarifa ya utendaji ya wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) kwa mwaka 2020/2021 jijini Dodoma.

  

SEHEMU ya washiriki wakifatilia wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi taarifa ya utendaji ya wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) kwa mwaka 2020/2021 jijini Dodoma.

…………………………………

Na Eva Godwin-DODOMA

SERIKALI imetangaza bei ukomo za huduma ya maji zitakazo anza kutumika katika maeneo ya vijijini ili kuleta unafuu kwa wananchi.

Bei hizo zilitangazwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) Prof. Idrisa Mshoro, katika hafla ya kukabidhi taarifa ya utendaji ya wakala huo kwa mwaka 2020/2021.

Pia, kusaini mikataba ya dira za maji za malipo kabla ya matumizi, kutangaza bei kikomo za huduma ya maji vijijini na ugawaji wa pikipiki kwa ofisi za Ruwasa.

“RUWASA kupitia kiako chake cha Bodi ya wakurugenzi kilichofanyika tarehe 25, Juni 2021 iliidhinisha bei za ukomo kwa vyombo vyote vya watoa huduma ya maji vijijini kwa kuzingatia teknolojia mbalimbali zinazotumika katika miradi ya maji vijijini baada ya kufanya tathimini ya kina ya bei zinazotozwa na vyombo vya watoa huduma ngazi ya jamii kwa sasa”alisema

Alisema bei kikomo zitakazo tumiwa na vyombo kwa wateja wenye dira za maji kwa miradi inayotumia nishati ya mafuta bei kikomo kwa uniti moja itakuwa Sh. 2,500 na ndoo ya lita 20 itauzwa Sh. 20 na wasaiyo kuwa na dira ya maji kwa mwezi itakuwa Sh. 15,000.

Kwa miradi ya maji inayotumia nishati ya umeme jua bei wa uniti moja itakuwa Sh.1500 na ndoo ya lita 20 itauzwa kwa Sh. 30 na wasaio na dira kwa mwezi itakuwa Sh.7,000.

“Miradi ambayo inatumia mserereko kufika kwa wateja itakuwa unit moja ni Sh. 1,000 na ndoo ya ujazo wa lita 20 itauzwa Sh.20 na kwa wasiokuwa na dira ya maji kwa mwezi itakuwa Sh. 5,000.

“Kwa umeme wa Tanesco uniti moja itakuwa Sh. 2,000 na ndoo ya lita 20 itauzwa Sh. 40, na kwa wasiokuwa na dira kwa mwezi itakuwa 10,000”alisema

Aidha, alisema kwa miradi inayotumia pampu za mkono uniti moja itakuwa Sh.1,000 na ndoo ya lita 20 itauzwa Sh.20 na kwa wasiokuwa na dira za maji itakuwa kwa mwezi Sh. 5,000.

Kwa maji ya jumla kutoka vyanzo vikuu uniti moja ni Sh. 2,500 na ndoo ya lita 20 ni sh. 50 na wasaiokuwa na dira za maji watalipa Sh. 15,000 kwa mwezi”alisema

“Aidha bei hizo zitaendana na masharti yafuatayo ikiwemo chombo chochote hakitaruhusiwa kutoza zaidi ya bei zilizoanishwa ”alisisitiza

Pia, alisema chombo chochote ambacho kinatoza bei chini ya bei kikomo kitaendelea kutoza bei ya awali na hakiruhusiwi kuongeza pasipo kupata idhini ya RUWASA.

Kadhalika, alisema chombo kinachotumia teknolojia zaidi ya moja katika uzalishaji wa maji kitatakiwa kutumia bei kikomo ya teknolojia inayochukua asilimia kubwa katika uzalishaji.

“Kufikia juni 30, 2022 vyombo vyote vinatakiwa kuwa vimefunga dira za maji kwa wateja wake wote. Kwa wateja wa majumbani na taasisi bei zitakuwa asilimia 70 ya bei kwa kila teknolojia kama zilivyoainishwa “alisema

Vilevile alisema bei kwa wateja wa bishara na viwanda zitabaki kama zilivyo ainishwa.

“Vyombo ambavyo vitashindwa kumudu gharama za uendeshaji na matengenezo ya miradi vinayosimamia kutokana na bei kikomo zilizoainishwa viwasailishe maombi ya bei maalum kwa kufuata utaratibu uliotolewa kwenye mwongozo wa upangaji bei mwaka 2020”alisema

Awali Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa wizara yake haitakua kikwazo katika kukwamisha upatikanaji maji safi na salama na kuposheleza.

‘Mameneja wa Ruwasa wilaya na mikoa hakikisheni mnafatilia miradi inayotekelezwa na Serikali ili kukamilika kwa wakati na wananchi kupata huduma ya maji ya uhakika’amesema Aweso

Pia amemshukuru Waziri wa Elimu kwa kufanya Mageuzi kwa kutumia vyuo vya ufundi kwa Majaribio ya kubuni na kutengeneza dira za Maji Nchini.

“Naibu Waziri wa Elimu tunaomba peleka salamu zetu kwa Waziri wa Elimu mageuzi aliyoyafanya ni makubwa sana na Wizara ya Elimu imekuwa ni msaada sana kwa Wizara ya Maji

” Hii ni fursa muhimu sasa kuhakikisha Mwananchi anaunganishiwa Dira ya Maji nyumbani kwake”.Amesema Aweso

Kwa upande wake  Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary  Kipanga amempongeza Waziri wa Maji kwa kuondoa changamoto ya usomaji wa Mita na kupunguza gharama kwenye eneo hilo pamoja na kuweka bei elezeki katika kila eneo la uzalishaji wa huduma.

“Leo tumeweza kujibu maswali ya watanzania kupitia tukio hili la leo na tunaamini watafurahi kwa tukio la leo

“Ninafuraha kuona Wizara ya Maji imetatua changamoto za watanzania, na sisi jukumu letu Wizara ya Elimu ni kuhakikisha tunasimamia tafiti hizi kwa maslai ya Wananchi na Taifa letu kwa ujumla”.Amesema Kipanga

Naye Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clement Kivegalo, amesema Ruwasa imekuja na mambo matatu ambayo ni unafuu wa uendeshaji wa Maji maeneo ya Vijijini ,kuboresha ukusanyaji wa mapato maeneo ya vijijini pamoja na kuboresha mbinu za malipo.

“Hali ya Maji vijijini ilikuwa ni mbaya sana tangu enzi na enzi lakini sahivi tunaona maendeleo makubwa yakifanyika nayanaendelea kufanyika” amesema Kivegalo

“Gharama za uendeshaji wa Maji Vijijini lazima uwe nafuu,Ruwasa tumekuja na maboresho makubwa kuanzia uboreshaji wa mapato, unafuu wa uendeshaji wa Maji pamoja na kuboresha mbinu za malipo”.Amesema Mhandisi Kivegalo

About the author

mzalendoeditor