Featured Kitaifa

CCM WILAYA YA BUTIAMA CHAWAPIGA MSASA VIONGOZI WAPYA WALIOCHANGULIWA KATIKA NGAZI YA MASHINA NA MATAWI.

Written by mzalendoeditor

Mbunge wa Jimbo la Butiama mkoani Mara, Mhe Jumanne Sagini akizungumza kwenye Semina ya Uongozi kwa Viongozi wa Mashina na Matawi ya Halmashauri ya Butiama

Mbunge wa Jimbo la Butiama mkoani Mara, Mhe Jumanne Sagini akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Mashina na Matawi ya Halmashauri ya Butiama.

………………………………

Na Mwandishi wetu,

Ikiwa chama cha mapinduzi (CCM) kikiwa kinaendelea na uchaguzi wa ndani ya chama katika ngazi mbalimbali kuanzia Mashina mpaka Taifa, Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Butiama, Hamisi Mkaruka Kura,aliandaa semina ya siku moja kwa viongozi wapya waliokwisha chaguliwa katika ngazi ya mashina na matawi ambao ni wenyeviti,makatibu na makatibu waenezi lengo likiwa ni kuwajengea uwezo viongozi hao namna ya kunadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuendelea kudumisha umoja ndani ya chama.

Aidha Mbunge wa Jimbo la Butiama Mheshimiwa Jumanne Sagini ameshiriki katika semina hiyo nakuwaomba viongozi hao kufanya kazi kwa uweledi na kuondokana na makundi ya ndani ya chama na badala yake kuyasemea maendeleo yanayofanywa na Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mbunge Sagini amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha na kuendeleza miradi ya maendelo mengi yenye tija na yanayosaidia kuleta huduma kwa wananchi wa jimboni humo.

Sagini ameweza kutaja baadhi ya maendeleo yaliyotekelezwa na yanaendelea kutekelezwa kuwa ni;- Afya,Elimu,Maji na Barabara,ambapo ameishukuru serikali kwa kutoa pesa nyingi ndani ya jimbo hilo ambazo zimeweza kukamilisha baadhi ya miradi iliyokuwa kitendawili kukamilika.

“Niliguswa sana kuja kugombea nafasi ya ubunge Butiama baada kuona wakati nikiwa RAS Simiyu nilishudia tukijenga miradi mingi na inakamilika kwa wakati” alisema

“Lakini niliumia sana kila nikija huku kwetu Butiama miradi inasuasua na mingine ipo kwenye mpango lakini haipati muafaka wa kuanza kutekelezwa kwa wakati mf;- ujenzi wa Hospital ya Wilaya ilikuwa imeshindikana kujengwa kutokana na mvutano wa baadhi ya watu kutaka ijengwe katika maeneo yao. Mimi nilimuomba mama Maria Nyerere akatupatia eneo la kutosha kujenga hosptali na Rais Samia kupitia fedha za uviko alitupatia pesa za kutosha na sasa ujenzi wa hospital hiyo uko umekamilika tunakamilisha mambo madogo madogo ili wananchi wetu waanze kupata huduma”

Hata hivyo aliendelea kuwasisistiza viongozi hao kuacha makundi na kushikamana kwa pamoja ili kuweza kufanya kazi kwa maendeleo zaidi ndani ya jimbo la Butima.

Pamoja na hayo Katibu wa Chama Wilaya ya Butiama aliwasihi viongozi hao kufanya vikao vya mara kwa mara katika maeneo yao kuyasemea yale ambayo serikali inatekeleza kupitia Ilani ya Chama na kusema hatashindwa kumchukulia hatua kiongozi aliechaguliwa na wanachama na akashindwa kutekaeleza majukumu yake atamuwajibisha kwa kufuata kanuni za Chama.

About the author

mzalendoeditor