Featured Kitaifa

UWEKEZAJI MKUBWA KUFANYWA NA SERIKALI KATIKA SEKTA YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI– MNDOLWA

Written by mzalendoeditor

 

Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa akiongea na
waandishi wa Habari baada ya mkutano na watumishi wa Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji na wahandisi wa Umwagiliaji wa Mikoa, uliofanyika Jijini
Dodoma mapema leo.

Mkurugenzi
Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa na Baadhi ya
watumishi wa Tume hiyo pamoja na wahandisi wa Umwagiliaji wa mikoa

Baadhi ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakifuatilia kikao kilichofanyika jijini Dodoma mapema leo.

Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw, Raymond Mndolwa amesema,
kutakuwa na kilimo cha umwagiliaji cha uhakika kutokana na uwekezaji
mkubwa wakihistoria unaofanywa na serikali ya awamu ya sita katika
sekta ya kilimo cha umwagiliaji.

Bw,Mndolwa ameyasema hayo mbele
ya Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dodoma mara baada
ya kufungua kikao kazi kilichowahusisha watumishi wote wa Tume ya Taifa
ya Umwagiliaji na kuongeza kuwa, kutokana na majukumu makubwa
iliyopewa na serikali Tume ya Taifa ya Umwagiliaji “niliona ni muhimu
sana tukutane watumishi wote ili tujipange,tuweze kutekeleza majukumu
hayo”.

“Tume tuna juku la kuwasaidia wakulima waweze kulima
kutokana na kilimo wanacholima ili waweze kupata maji katika mazao
wanayolima hili ni sehemu ya majukumu yetu, kutokana na hali yakuwa na
upungufu wa mvua serikali imeweka msisitizo mkubwa katika kilimo cha
umwagiliaji kwa matarajio yajayo”.

Tunataka Wananchi na Wakulima
waliokata tamaa ya kulima warudi shambani, kwasababu tume ya Taifa ya
Umwagiliaji imewezeshwa na inakuja kufanya mageuzi makubwa katika sekta
ya kilimo cha Umwagiliaji.

Akizungumzia suala la Bajeti kubwa
iliyoelekezwa na Serikali ya awamu ya sita katika Sekta ya Kilimo cha
Umwagiliaji, Mkurugenzi Mndolwa ameongeza kusema kuwa, Tume imeelekeza
nguvu katika miradi iliyokwisha buniwa na miradi hiyo ndiyo ya
kipaumbele, baada ya miradi hiyo ya mwaka huu hatua itakayofuata ni
kujenga miradi mingine ya umwagiliaji nchini katika maana ya mikoa yote
itakayotekeleza kilimo cha umwagiliaji na aina gani ya miradi ifanyike
katika kuhakikisha kila Mkoa na Wilaya inapata miradi ya Kilimo cha
Umwagiliaji.

Alisema wana panga upya kuhakikisha kwamba mwaka wa fedha unaofuata yaani 23/24 watakuwa na mkakati ambao utaenea nchinzima.

Mwaka
wa fedha huu 22/23 watarekebisha Skimu thelathini (30) za kilimo cha
umwagiliaji lakini Wahandisi wa umwagiliaji wa mikoa watafanya mapitio
ya miradi iliyokwisha kwa lengo la maboresho kulinga na na bajeti yetu.

“Nina
ahidi kwamba maboresho yatakuwa makubwa ili kila mwananchi anayetaka
kulima aweze kulima.”Alisisita Kikao cha leo ni majumuisho ya siku
yapili ya kikao kilichohusisha watumishiwa Tume Makao makuu na
Wahandisi wa Umwagiliaji wa mikoa kilichojadili, Mpango mkakati wa
miaka mitano wa utekelezaji wa shughuli zaTume.

About the author

mzalendoeditor