Featured Kitaifa

WAZIRI NAPE ATAKA WAZAZI NA WALEZI KUWALINDA WATOTO DHIDI YA MATUMIZI YA TEHAMA 

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye ,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya TEHAMA katika shule ya Sekondari ya Chinangali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ambavyo vimetolewa  Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) jijini Dodoma.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mkuu wa Idara ya Ununuzi na Ugavi wa mfuko huo, John Munkondya,akizungumzia jinsi wanavyotekeleza mradi wao wa kugawa vifaa vya TEHAMA kwa shule za msingi na Sekondari lengo la kukuza matumizi ya TEHAMA nchini.

Mbunge wa Dodoma Mjijni, Mhe. Anthony Mavunde,akiipongeza UCSAF kwa kuendelea kuwajali wanafunzi nchini.

AFISA Elimu Sekondari jiji la Dodoma,Upendo Rweyemamu,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya TEHAMA katika shule ya Sekondari ya Chinangali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ambavyo vimetolewa  Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) jijini Dodoma.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Chinangali, Victor Salisali ,akiishukuru Serikali kwa kupeleka vifaa hivyo vya TEHAMA katika Shule hiyo ambavyo vitasaidia kupanua wigo wa matumizi ya TEHAMA na kuimarisha mifumo ya utendaji wa walimu na wanafunzi.

SEHEMU ya Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chinangali wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya TEHAMA katika shule ya Sekondari ya Chinangali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ambavyo vimetolewa  Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akikabidhiwa shairi na wanafunzi wa  shule ya Sekondari Chinangali alipofika shuleni hapo  kukabidhi vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa na  Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akitoa zawadi baada ya kuuliza swali kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chinangali baada ya kujibu swali la historia ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika alipofika shuleni hapo kukabidhi vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa na  Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (kulia) Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde (kushoto) wakikabidhi vifaa vya TEHAMA kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Chinangali vilivyotolewa na  Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wanafunzi na walimu wa Shule ya Sekondari Chinangali mara baada ya kukabidhi vifaa vya TEHAMA kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Chinangali vilivyotolewa na  Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) jijini Dodoma.

………………………………

Na Eva Godwin-DODOMA

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye ,amewataka Wazazi na Walezi kuwalinda Watoto wao na kuwaambia ukweli kuhusu faida na hasara za ya matumizi ya intanenti yanayotokana na ukuaji wa  TEHAMA.

Kauli hiyo ameitoa Juni 16 jijini Dodoma,wakati akigawa vifaa vya TEHAMA katika shule ya Sekondari ya Chinangali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ambavyo vimetolewa  Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kuendelea kuwapatia watoto wa kitanzania nafasi ya kujifunza na kutumia TEHAMA.

Waziri Nape amesema kuwa lazima wazazi au walezi wawambie watoto kuhusu matumizi ya intanenti yanayotokana na ukuaji wa  TEHAMA ambayo ikitumika visivyo huchangia kuharibu mila na desturi za kitanzania kwa kufuata tamaduni za kigeni zinazokinzana na maadili ya kitanzania

“Tuwalinde watoto kwa kuwaambia ukweli kwasababu akiharibika ni wajibu wa Mzazi au Mlezi ,watoto wamekuwa na Uhuru ambao unawaaribu kisaikolojia”,Amesema Nape

“Sisi Serikali tutafanya wajibu wetu na tutachukua hatua zetu za kuwalinda Watoto hasa Mashuleni na Mazingira ambayo siyo salama kwao”

Hata hivyo Waziri Nape amesema kuwa Serikali imewekeza kwenye miundombinu ya elimu ikiwa ni sehemu ya kumuandaa mtoto wa Kitanzania kuchukua dhamana ya kuijenga nchi, ikiwa ni pamoja na elimu ya matumizi ya TEHAMA ambayo hayaepukiki katika ulimwengu wa kidijitali. 

“Kama ilivyo maisha bila moto haiwezekana lakini ukitumika vibaya unaweza kuleta madhara makubwa hata kupoteza maisha vivyo hivyo TEHAMA ikitumika vibaya inaweza kumuathiri mtoto wa kiafrika kujifunza tamaduni zisizofaa na matendo ya uovu kupitia mtandao hasa intaneti”, 

“Wizara ninayoisimamia ina wajibu wa kuhakikisha kunakuwa na matumizi salama ya mtandao, lakini pia ni wajibu wa wazazi na walezi wakiwemo walimu kuwalinda watoto wetu dhidi ya changamoto zinazotokana na ukuaji wa TEHAMA na kwa kuchungulia nini watoto wanafanya kwenye mtandao na kutoona aibu kuwaeleza ukweli juu ya faida na hasara za ukuaji wa TEHAMA”.

Kwa upande wake  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mkuu wa Idara ya Ununuzi na Ugavi wa mfuko huo, John Munkondya amesema kuwa ugawaji wa vifaa vya TEHAMA kwa shule za msingi na Sekondari ni moja ya mradi unaotekelezwa na mfuko huo kwa lengo la kukuza matumizi ya TEHAMA nchini 

“Kupitia Mbunge wetu Antony Mavunde leo hii shule yetu ya Chinangali inakabidhiwa vifaa vya TEHAMA hakika tunashukuru sana Waziri Nape 
“Vifaa hivi pia ni utekelezaji wa Mradi wetu wa kuunganisha shule kupitia vifaa hivi  vya TEHAMA,”Amesema Mkondya.

Awali Mbunge  wa Dodoma Mjijni, Mhe. Anthony Mavunde,amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa kutoa  Elimu bure kwa Kidato cha Tano na Cha Sita

“Juzi kwenye Bajeti Mh.Rais amewafuta Machozi Wazazi Wengi wanaosomesha watoto  Hasa wa Kidato cha Tano na cha Sita ya kwamba Ada haitokuwepo tena hii ni hoja ambayo aliipendekeza

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Chinangali, Victor Salisali ameishukuru Serikali kwa kupeleka vifaa hivyo vya TEHAMA ambavyo vitasaidia kupanua wigo wa matumizi ya TEHAMA na kuimarisha mifumo ya utendaji wa walimu na wanafunzi

About the author

mzalendoeditor