Featured Michezo

WAZIRI MCHENGERWA AIPONGEZA TIMU YA WANAWAKE YA KRIKETI KWA KUONGOZA RWANDA

Written by mzalendoeditor


Na John Mapepele
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza
timu ya Tanzania ya  Wanawake ya Kriketi kwa kufanya vizuri na kuongoza
kwenye mashindano ya Kwibuka Cup yanayoendelea nchini hivi sasa nchini
Rwanda.
Mhe. Mchengerwa ametoa pongezi hizo leo Juni 15, 2022 alipoongea na simu timu hiyo kupitia kwa Nahodha wa timu hiyo .
Amesema
anaipongeza timu hiyo  baada ya kuzishinda timu zote walizokutana nazo
kwenye mashindano hayo na kuwa kinalani mwa mashindano hayo.
Amezitaja
timu hizo kuwa ni Kenya, Uganda, Rwanda, Botswana na  Ujerumani  bado
timu ya Nigeria na Brazil ambapo wakishinda mechi mojawapo wanaingia
fainali za mashindano hayo.
Aidha,
amemshukuru Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mhe.  Meja Jenerali
Richard Makanzo  kwa kuwa karibu na timu hiyo katika kipindi chote huku
akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuisaidia timu hiyo ili ifike mbali
zaidi.

About the author

mzalendoeditor