Featured Kitaifa

VIONGOZI WA UMMA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU.

Written by mzalendoeditor

Kamishna wa Maadili Mh Jaji wa rufani Sivangilwa Mwangesi,akizungumza wakati wa kikao  chake na Viongozi wa Mkoa wa Mwanza wakati wa  maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza leo Juni 16,2022.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi  Robert Gabriel ,akizungumza wakati wa  maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kilichofanyika katika Ofisi yake  leo Juni 16,2022 jijini Mwanza.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Kamishna wa Maadili Mh Jaji wa rufani Sivangilwa Mwangesi (hayupo pichani),wakati wa kikao  chake na Viongozi wa Mkoa wa Mwanza wakati wa  maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza leo Juni 16,2022.

Kamishna wa Maadili Mh Jaji wa rufani Sivangilwa Mwangesi,akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza mara baada ya kikao  chake na Viongozi wa Mkoa wa Mwanza wakati wa  maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza leo Juni 16,2022.

………………………………………

Na Mwandishi Wetu-DODOMA
Kamishna wa Maadili Mh Jaji wa rufani Sivangilwa Mwangesi amewataka Viongozi wa Umma kufanya kazi kwa Uadilifu na kutojiingiza ktk vitendo vinavyopelekea ukiukwaji wa Maadili.
Mh Mwangesi ameyasema hayo leo Juni 16,2022 katika Kikao chake na Viongozi wa Mkoa wa Mwanza wakati wa  maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Mh Mwangesi amewaasa Viongozi hao kitojiingiza katika mgongano wa Maslahi jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
‘Viongozi watawajibika katika maeneo yao ya kazi kwa uadilifu itapelekea kujenga imani kwa wananchi wanaowaongoza na Serikali kwa ujumla.”amesema Mwangesi

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi  Robert Gabriel,amesema  kuwa Maadili ni hatua muhimu inayo tambulisha mtu ndani ya Jamie husika na maadili hujitokeza ktk matendo yake.
‘Lengo la kikao hiki ni kuunga mkono jitiihada za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan katika kupinga vitendo vya Rushwa, Ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za Umma.’amesema Mhandisi Gabriel
Maadhimisho hayo ya Wiki ya Utumishi wa Umma nchini yameanza rasmi Leo tar 16 juni na yatahitimishwa Juni 23, 2022

About the author

mzalendoeditor