Featured Kitaifa

IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO BAADHI YA MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA

Written by mzalendoeditor

Ndugu waandishi wa habari,

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon N. Sirro, tarehe 15.06.2022 alifanya uhamisho wa baadhi ya maofisa kwa lengo la kuboresha ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Jeshi la Polisi.

Ndugu waandishi wa habari,

Waliohamishwa ni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) William F. Mkonda aliyekuwa Kamanda wa Polisi Tarime Rorya anayekwenda kuwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salam (ZTO) akichukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdi H. Isango ambaye anakwenda kuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Mbeya. 

Ndugu waandishi wa habari,

Pia amemuhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Zuberi Mwombeji ambaye alikuwa Mkuu wa Operesheni Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwenda Makao Makuu ya Polisi kuwa Mkuu wa Kitengo cha Ustawi wa Jamii na Uchumi, na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Kennedy P. Mgani ambaye alikuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Mbeya. 

Aidha amemuhamisha Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Pipi J. Kayumba kwenda Mkoa wa Singida kuwa Afisa Mnadhimu namba moja na nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Tarcis M. Idelfonce ambaye alikuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma.  

Ndugu waandishi wa habari,

IGP Sirro pia amemhamisha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Jumanne I. Juke aliyekuwa Mkuu wa Polisi wilaya ya Geita kwenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi Rufiji kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ame A. Anoqie ambaye amehamishiwa Tarime Rorya kuwa Afisa Mnadhimu namba Moja kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Geofrey B Sarakikya ambaye anakuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa  Kipolisi Tarime/Rorya. 

Imetolewa na:                                                              

David A. Misime – SACP

Msemaji wa Jeshi la Polisi             

Makao Makuu ya Polisi

Dodoma, Tanzania 

About the author

mzalendoeditor