Featured Michezo

MWIGULU NCHEMBA AIPONGEZA YANGA BUNGENI, AWAMWAGIA SIFA FEI TOTO,MAYELE

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2022/23, bungeni, jijini Dodoma.

……………………………………….

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba ameipongeza klabu ya Yanga kwa mwenendo wao mzuri Msimu huu

Mwigulu Nchemba ametoa Pongezi hizo wakati akiwasilisha Bajeti kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 Bungeni jijini Dodoma

“Nitumie fursa hii kumwomba radhi Bosi wangu Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kitendo alichowafanyia mwanangu Fei Toto kule Mwanza. Mniwie radhi, nilipompeleka FEI TOTO Yanga sikujua atakuja kuwafanyia kitumbaya hivi, mpaka nasikia anatafutwa maliasili eti kaua mnyama bila kibali.

“Nakupongeza Mheshimiwa Anthony Mavunde wewe ndio ulikuwa Mwenyekiti wa kuisaidia Yanga ikiwa na mapito. Nampongeza GSM kwa kurejesha furaha ya wananchi hasahasa kwa udajili wa Fiston Mayele. Mayele amekuwa maarufu kuliko Makatibu wenezi wa baadhi ya vyama vya Siasa.”

“Nawapongeza sana na marafiki zangu klabu ya Simba kwa kuwakilisha vyema kwenye mashindano ya Kimataifa, wananijua mara zote kimataifa tuko pamoja, siwezi kukana Bendera ya Taifa langu kwa ajili ya utani wa jadi” – Mwigulu Nchemba

About the author

mzalendoeditor