Na Eva Godwin-DODOMA
MKUU wa kitengo cha utafiti wa Mipango NACTVET Dkt. Obeid Mahenya amewashukuru wananchi Mkoa wa Dodoma kwa kuonyesha ushirikiano tangu kuanza kwa maonyesho mpaka kumalizika kwa maonyesho hayo.
Akizungumza na Mzalendo blog June 13, mwaka huu katika maonyesho ya NACTVET ikiwa ni siku ya mwisho ya kufunga maonyesho hayo.
Amese Mukhitikio umekuwa mkubwa tofauti na miaka mingine na watu wameonyesha juhudi katika kuonyesha bunifu zao mbalimbali
“Tumefarijika sana tumeona mukhitikio mkubwa sana kwa wakazi wa Dodoma na pia tumeona bunifu zao mbalimbali ambazo wamezionyesha mwanzo wa maonyesho mpaka leo ambapo yamemalizika “,amesema Mahenya
” Tumeona pia baadhi ya vyuo mbalimbali ambavyo wamepata tuzo kwa kuonyesha juhudi ambazo wamefanya Tangu maonyesho kuanza na mpaka leo kumalizika”
Lakini pia Dkt.Mahenya Licha ya kuwashukuru Wakazi wa Dodoma amevishukuru vyuo mbalimbali ambavyo vimeshiriki katika kutoa huduma katika uwanja wa Maonyesho.
“Tumeona vyuo vya afya vikitoa huduma ya kupima presha,Damu,uzito na magonjwa Mengine
” Kwa ujumla vyuo takribani vyingi vimejitahidi kuonyesha ujuzi wao katika maeneo mbalimbali na pia watu wengi wamejifunza kupitia maonyesho haya”.Amesema Mahenya