Featured Michezo

DUCE YAWAKUTANISHA WATUMISHI KWENYE BONANZA LA MICHEZO

Written by mzalendoeditor

Watumishi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) “Team Yellow” wakishangilia wakiwa na baadhi ya medali na makombe baada ya kuwashinda wenzao “Team Blue” katiika michezo mbalimbali kwenye Bonanza lililowakutanisha watumishi wa Chuo hicho kwenye viwanja vya Gwambina Temeke leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam. Watumishi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakishangilia wakiwa na baadhi ya medali na kombe baada ya kuwashinda wenzao Team B katiika michezo mbalimbali kwenye Bonanza lililowakutanisha watumishi wa Chuo hicho kwenye viwanja vya Gwambina Temeke leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) , Prof.Stephen Maluka akimvalisha medali Naibu Rasi , Taaluma,Utafiti na Ushauri elekezi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Dkt.Christina Raphael wakati wa Bonanza lililowakutanisha watumishi wa Chuo hicho kwenye viwanja vya Gwambina Temeke leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) akiwakabidhi vyeti baadhi ya Watumishi wa Chuo hicho mara baada ya kufanya vizuri kwenye taasisi katika idara mbalimbali kwenye taaluma kwa mwaka uliopita.

Mkuu wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.Stephen Maluka akikabidhi zawadi kwa watumishi wa Chuo hicho waliofanya vizuri kwenye Bonanza la michezo lililowakutanisha watumishi wa Chuo hicho kwenye viwanja vya Gwambina Temeke leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya watumishi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakishiriki mchezo wa Netball kwenye Bonanza la michezo lililowakutanisha watumishi wa Chuo hicho kwenye viwanja vya Gwambina Temeke leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya watumishi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakishiriki mchezo wa Volleyball kwenye Bonanza la michezo lililowakutanisha watumishi wa Chuo hicho kwenye viwanja vya Gwambina Temeke leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya watumishi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakishiriki mchezo wa kukimbia na gunia kwenye Bonanza la michezo lililowakutanisha watumishi wa Chuo hicho kwenye viwanja vya Gwambina Temeke leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya watumishi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakishiriki mchezo wa drafti kwenye Bonanza la michezo lililowakutanisha watumishi wa Chuo hicho kwenye viwanja vya Gwambina Temeke leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya watumishi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakishiriki mchezo wa bao kwenye Bonanza la michezo lililowakutanisha watumishi wa Chuo hicho kwenye viwanja vya Gwambina Temeke leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.Stephen Maluka (kushoto) akishuhudia mchezo wa karata kati ya Naibu Rasi (Utawala, Fedha na Mipango) Dkt.Method Samwel akicheza na Naibu Rasi (Taaluma,Utafiti na Ushauri elekezi) Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Dkt.Christina Raphael kwenye Bonanza la michezo lililowakutanisha watumishi wa Chuo hicho kwenye viwanja vya Gwambina Temeke leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.Stephen Maluka  akizungumza kwenye Bonanza la michezo lililowakutanisha watumishi wa Chuo hicho kwenye viwanja vya Gwambina Temeke leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.Stephen Maluka (katikati) akizungumza kwenye Bonanza la michezo lililowakutanisha watumishi wa Chuo hicho kwenye viwanja vya Gwambina Temeke leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Rasi (Utawala, Fedha na Mipango) Dkt.Method Samwel akizungumza kwenye Bonanza la michezo lililowakutanisha watumishi wa Chuo hicho kwenye viwanja vya Gwambina Temeke leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Michezo (DUCE), Dkt.Samwel Mhajida akizungumza kwenye Bonanza la michezo lililowakutanisha watumishi wa Chuo hicho kwenye viwanja vya Gwambina Temeke leo Juni 11,2022 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mkuu wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Prof.Stephen Maluka amehimiza kamati ya michezo ya Chuo hicho kuhakikisha kunakuwepo na utaratibu wa ufanyaji mazoezi kwa watumishi ili ifikapo siku ya michezo waweze kushiriki ipasavyo na kuweza kuimarisha afya zao.

Ameyasema hayo leo Juni 11, 2022 wakati wa Bonanza maalumu la Wafanyakazi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam,(DUCE) lililofanyika katika viwanja vya Gwambina Temke Jijini Dar es Salaam.

Amesema katika tamasha hilo wameweza kufanya mazoezi na kuimarisha afya zao lakini pia wamepata  nafasi ya kutambuana na kufahamiana zaidi hivyo basi michezo hiyo ikiendelea litakuwa jambo zuri na lenye manufaa kwa taasisi.

“Tunapokutana pamoja kwenye mazingira kama haya yanaondoa ile hali ya huyu bosi, huyu sio bosi,, leo tumepata nafasi kwa pamoja, jambo zuri sana hili. Amesema Prof.Maluka.

Aidha amesema wameridhia wao kama menejimenti kutenga siku moja kwa mwezi kwaajili ya michezo ambapo kila Alhamisi ya mwsisho wa mwezi itakuwa siku ya michezo kwa Chuo hicho.

“Kwakuona umuhimu wa michezo, tulikaa na kamati ya michezo wakatupa ushauri sisi menejimenti, tukachukua baadhi ya ushauri na moja ya ushauri ambao tumeuchukua ni kuwepo kwa sare ya taasisi na tukalifanyia kazi”. Amesema 

Kwa upande wake Mratibu wa Michezo (DUCE), Dkt.Samwel Mhajida amesema kupitia bonanza hilo wameweza kukutana pamoja kama watumishi na kufurahi pamoja na kushrikishana katika mambo ambayo sio ya kitaaluma na ya kikazi.

Amesema ni bonaza ambalo pia ambalo linawatambua watu ambao walifanya vizuri kwa mwaka uliopita kwa maana wafanyakazi bora katika taasisi kwenye idara mbalimbali ambao wamepatiwa zawadi kwa kutambua mchango wao.

About the author

mzalendoeditor