Featured Kitaifa

NIT MBIONI KUTOA MAFUNZO YA URUBANI

Written by mzalendoeditor

Naibu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Dk.Prosper Mgaya, akizungumza katika banda la Chuo hicho katika maonesho ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yanayoendelea uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma

………………………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)  kipo mbioni kuanza kutoa mafunzo ya urubani .

Pia,kimesema  kimejipanga kuzalisha wataalamu wengi katika nyanja za usafiri wa anga na majini kutokana na Serikali kuongeza meli na ndege.

Hayo yameelezwa leo June 9,2022  na  Naibu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Dk.Prosper Mgaya,wakati akizungumza katika banda la Chuo hicho katika maonesho ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yanayoendelea uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma

Dk Mgaya, amesema mafunzo hayo yataanza  mwezi ujao mara baada ya ndege kufika na kukaguliwa na Mamlaka zinazohusika.

“Wakufunzi wapo South Afrika na hivi karibuni watafika kutoka katika mafunzo hayo.Tumeajiri wakufunzi ambao  walikuwa ni wastaafu  wafanyakazi katika Shirika la Ndege ambao ndio tulianza nao.

“Tumeishakaguliwa katika stage nne za  mwanzo ambazo sasa imebaki ‘demostartion’ hapo wanakuja kuona vifaa na TCRA ni lazima wakague.

“Tunaishukuru Serikali inatusaidia sana na tumepata mradi ambao utasaidia katika mafunzo ya usafiri wa anga ni gharama kubwa na chuo kisingeweza,”amesema Dk Mgaya,

Aidha,amesema wamejipanga  kuzalisha wataalamu wengi katika nyanja za usafiri wa anga na majini kutokana na Serikali kuongeza meli na ndege.

“Kwa sasa tuna mafundi na Serikali tunaongeza ndege pamoja na meli tunahitaji mafundi ndio maana tumeanzisha kozi ya utengenezaji wa ndege,haya ni mafunzo maalum kwahiyo tunawaandaa vijana wetu kufanya mitihani yenye leseni,”amesema

Pia amesema wana mafunzo kwa ajili usanifu wa meli lengo lengo likiwa ni kuongeza idadi ya wataalamu kutokana na Serikali  kununua na kutengeneza meli nyingi.

“Nchi yetu imezungukwa na maji na kuna maboti hivyo tumeona tuende huko na tuna boti ya Kisasa kule Nyasa tunawasaidia wavuvi wadogo wadogo ili kutoa watu wenye umahiri,”amesema.

Kuhusu kozi ya  madereva,Dk Mgaya, amesema wanaendesha mafunzo ya kuwajengea uweledi ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto za ajali ambazo zimekuwa zikitokea.

“Tumetengeneza mtaala kwa kuwatumia madereva wetu na watakuwa na umahiri katika kupunguza ajali,”amesema.

About the author

mzalendoeditor