Featured Kitaifa

MKUTANO WA 114 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA OACPS WAFANYIKA BRUSSELS

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine akiongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 114 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya OACPS unaofanyika jijini Brussels, Ubelgiji akimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na Rais wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) Mhe. Sylvie Baïpo Temon (katikati) akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa 114 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo jijini Brussels nchini Ubelgiji. 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine akiwa katika Mkutano wa 114 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya OACPS unaofanyika  jijini Brussels, Ubelgiji akimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mulamula.Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mhe. Jestas Nyamanga na kulia ni Bi Agness Kiama akimwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Baadhi ya washiriki  kutoka nchi wanachama Jumuiya ya OACPS wakifuatilia ufunguzi wa mkutano Mkutano wa 114 wa Baraza la Mawaziri wa jumuiya hio unaofanyika jijini Brussels nchini Belgium

Baadhi ya washiriki  kutoka nchi wanachama Jumuiya ya OACPS wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika jijini Brussels nchini Belgium

……………………………..

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine anamwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika mkutano wa 114 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki (OACPS) unaofanyika jijini Brussels, Ubelgiji.

Mkutano huo wa siku mbili unajadili masuala mbalimbali ukiwemo mustakakabali wa maendeleo ya Jumuiya hiyo na namna nchi wanachama zinavyoweza kuendelea kukuza ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo na Umoja wa Ulaya, ambaye ni mbia wa maendeleo wa muda mrefu.

Mkutano huo pia unajadili maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya hiyo unaotarajiwa kufanyika mwezi Desemba, 2022 nchini Angola.

Akizungumza katika kikao hicho, Balozi Sokoine amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Jumuiya ya OACPS katika kuhakikisha vipaumbele vya nchi vinatekelezwa hususan katika sekta za kilimo, viwanda na biashara, uvuvi na madini ili nchi iweze kunufaika.

Mkutano huo unakutanisha nchi wanachama 79 wa Jumuiya hiyo ambao kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili wajumbe wake wanakutana ana kwa ana tangu dunia ilipokumbwa na janga la  UVIKO 19, wajumbe wengine  walioshindwa kuhudhuria wanashiriki kwa njia ya mtandao.

Baraza la Mawaziri la nchi wanachama wa OACPS ni chombo cha maamuzi cha Jumuiya hiyo ambacho kinahusika na utekelezaji wa maazimio yanayopitishwa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali.

Baraza hilo linaundwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka kwa Nchi wanachama na hukutana mara mbili kwa mwaka kujadili utekelezaji wa maazimio  yaliyofikiwa kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya hiyo.

About the author

mzalendoeditor