Featured Kitaifa

AQRB : TUMIENI WATAALAMU KATIKA UJENZI

Written by mzalendoeditor

Mbunifu wa Majengo Mwandamizi kutoka Bodi ya Usajili  wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  (AQRB) Pantaleo Mwamba wakati akizungumza leo Juni 9,2022 katika maonesho  ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yanaendelea Jijini Dodoma.

Mbunifu wa Majengo Mwandamizi kutoka Bodi ya Usajili  wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  (AQRB) Pantaleo Mwamba ,akionyesha vifaa vilivyopo katika Banda hilo wakati akizungumza leo Juni 9,2022 katika maonesho  ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yanaendelea  uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Afisa Uhusiano wa Bodi hiyo,Atugonza Samweli,akieleza namna walivyojipanga kutoa elimu katika Banda hilo katika maonesho  ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yanaendelea  uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

…………………………………………….

Na Alex Sonna-DODOMA

Bodi ya Usajili  wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  (AQRB) imeshauri watanzania kujenga kwa kufuata ushauri wa wataalamu.

Hayo yameelezwa leo Juni 9,2022 na Mbunifu wa Majengo Mwandamizi,Pantaleo Mwamba wakati akizungumza katika maonesho  ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yanaendelea Jijini Dodoma.

Mwamba amesema  wanashauri wananchi wafike kwa wingi  katika banda la Bodi hiyo  kwa sababu watapata elimu ya kujenga kwa kufuata taratibu na ni  taratibu zipi zinatakiwa  kufuata.

“Na wataalamu utawapataje na wanafanya kazi gani ukija katika banda letu tutakupa elimu jinsi ya kuanza kutafuta ramani pamoja na kwanini unatakiwa kujenga kwa kufuata taratibu,”amesema.

Amesema wapo katika maonesho hayo kwa ajili ya kutoa elimu pamoja na shughuli zinazofanywa na Bodi hiyo.

“Kuna hatua za kufuata mpaka kufikia katika ujenzi  ni lazima ufanye ubunifu ndio uje na ramani ndio unakuja kutengeneza mfano wa jengo,”amesema.

Amesema kazi za mbunifu majengo pia ni kusimamia ujenzi  mwanzo hadi mwisho.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Bodi hiyo,Atugonza Samweli amesema kwa sasa ofisi za Bodi hiyo rasmi zimehamia Jijini Dodoma.

“Niwatangazie Wananchi ofisi zetu za Makao Makuu zimehamia Dodoma ofisi ndogo ndio itabaki Dar es salaam,”amesema.

About the author

mzalendoeditor