Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Mh Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto ) akisalimiana na Bw Madaraka Nyerere ambae ni mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipowasili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa Kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika leo chuoni hapo.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Mh Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kushoto ) akiwaongoza viongozi mbalimbali wa kisiasa, kitaaluma na kiserikali wakati wa maandamano mafupi kueleka ukumbuni kwa ajili ya uzinduzi wa Kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika leo chuoni hapo. Wengine ni pamoja na Waziri Mkuu mstaafu Mh Mizengo Pinda (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu, Profesa Rwekaza Mukandala,(wa tatu kulia), Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa William Anangisye (Kushoto) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga (Kulia).
Maofisa wa Benki ya NBC tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwemo Meneja Maendeleo Biashara tawi hilo Bw Fredrick Massawe (Kulia) na Ofisa Mauzo wa tawi hilo Bw Amir Mhina wakiwahudumia baadhi ya wateja ambao ni wanafunzi wa Chuo hicho, Bi Anna Kipuzi na Maria Kipuzi waliotembelea banda la maonesho ya huduma za benki hiyo lilipo nje ya ukumbi wa Kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere chuoni hapo.
Maofisa wa Benki ya NBC tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwemo Meneja Maendeleo Biashara tawi hilo Bw Fredrick Massawe (Kulia) na Ofisa Mauzo wa tawi hilo Bw Amir Mhina wakiwahudumia baadhi ya wateja ambao ni wanafunzi wa Chuo hicho waliotembelea banda la maonesho ya huduma za benki hiyo lilipo nje ya ukumbi wa Kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere chuoni hapo.
Sehemu ya washiriki wa Kongamano la 13 la Kigoda Cha Mwalimu Nyerere akiwemo Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bi Anne Mwaisaka wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kongamano hilo chuoni hapo.
……………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeshiriki kikamilifu kwenye uzinduzi wa Kongamano la 13 la Kigoda Cha Mwalimu Nyerere uliofanyika leo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Kongamano hilo la siku tatu limezinduliwa na Mkuu wa Chuo hicho, Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Mh Jakaya Mrisho Kikwete, ambae aliongoza viongozi mbalimbali wa kisiasa, kitaaluma na kiserikali akiwemo Waziri Mkuu mstaafu Mh Mizengo Pinda.
Mbali na kuwa mmoja wa wadhamini muhimu katika kongamano hilo, Benki ya NBC kupitia tawi lake la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliweza kuandaa banda maalum kwa ajili ya kutoa huduma zake kwa washiriki wa kongamano hilo sambamba na kushiriki katika kongamano hilo.
“Benki ya NBC tunatambua mchango na farsafa za Hayati Mwalimu Julius Nyerere si tu kitaifa bali pia katika uanzishwaji wa benki hii. Hii imekuwa ni moja ya sababu muhimu kabisa ya sisi kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kufanikisha na kushiriki katika masuala yote yanayohusiana na Hayati Mwalimu Julius Nyerere likiwemo Kongamano hili muhimu,’’ alisema Bi Anne Mwaisaka, Meneja wa Benki ya NBC Tawi la chuo hicho.