Featured Kitaifa

DK GWAMAKA ATAJA MIKAKATI YA NEMC

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira  (NEMC) Dkt.Samuel Gwamaka,akielezea mikakati waliyonayo katika kukabiliana na changamoto za uharibufu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini mara baada ya kumalizika kwa Maonyesho ya  Wiki ya Mazingira jijini Dodoma.

Mkutubi kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Cecilia Doualas,akitoa maelezo kwa wanafunzi pamoja wananchi waliotembelea Banda la NEMC katika viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini Dodoma wakati wa maonesho ya wiki ya mazingira yaliyomalizika Dodoma.

AFISA Elimu ya Jamii kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Suzan Chawe,akitoa maelekezo kwa mwananchi aliyetembelea Banda la NEMC katika viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini Dodoma wakati wa maonesho ya wiki ya mazingira yaliyomalizika Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -Tamisemi (Elimu), Dk Charles Msonde,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Banda la NEMC katika viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini Dodoma wakati wa maonesho ya wiki ya mazingira yaliyomalizika Dodoma.

WANANCHI mbalimbali wakiendelea kupata elimu katika Banda la NEMC katika viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini Dodoma wakati wa maonesho ya wiki ya mazingira yaliyomalizika Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira  (NEMC) Dkt.Samuel Gwamaka,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuelezea  mikakati waliyonayo katika kukabiliana na changamoto za uharibufu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini mara baada ya kumalizika kwa Maonyesho ya  Wiki ya Mazingira jijini Dodoma.
……………………………………

Na Alex Sonna _Dodoma
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira  (NEMC) Dkt.Samuel Gwamaka ametaja mikakati waliyonayo katika kukabiliana na changamoto za uharibufu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza Jijini Dodoma katika maonesho ya mazingira,Dk.Gwamaka  amesema hali ya mazingira nchini siyo nzuri hivyo wameweka mikakati ya kutoa elimu kwa wananchi, kusimamia Sheria na Kanuni ikiwemo kuwapa adhabu kali wale wanaofanya vitendo vya uharibifu wa mazingira.

“Mkakati wa  kuelimisha umma  nia yetu wananchi kutii Sheria bila shuruti na hili linakuja kwa kutoa elimu mtu akikata miti ahakikishe anapanda miti, pia suala la taka  ngumu na makelele imekuwa ni changamoto,”amesema.

Aidha Dk.Gwamaka amesema sababu za uharibifu wa mazingira  ni ongezeko la watu, misitu kuvamiwa na shughuli za binadamu kuendelea katika maeneo ya vyanzo vya maji.

“ Sehemu ya vyanzo vya maji vimevamiwa yale maeneo yaliyotengwa mita 60 wameshindwa kuyalinda   na baadhi ya watu wanatumia kilimo cha umwagiliaji kutoka mtoni.Ukienda Kigoma,Katavi,Mtwara kuna shughuli kubwa za kibinadamu zinaendelea hali siyo nzuri kwa upande wa rasilimali za misitu.

“Kumekuwa na ongezeko la mimomonyoka ya udongo  hivyo mito yetu kujaa udogo na katika milima ambayo ilikuwa ni hifadhi sehemu kubwa zimevamia Mbeya, Uruguru hata kule Usambaani maeneo makubwa yamevamiwa.Mvua zikinyesha hakuna utulivu wa maji hivyo kumekuwa na mafuriko,”amesema Dk.Gwamaka

“Tumekuwa tukitoa elimu kwa viongozi wa dini na kwa wamiliki wa kumbi za starehe, maeneo mengine utupaji wa taka ngumu zote hizo ni changamoto,”amesema.

Mkurugenzi huyo amezitaja hatua ambazo wamechukua wakizichukua ni pamoja na kuwapiga faini wale wenye makosa pamoja na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi.

About the author

mzalendoeditor