Featured Kitaifa

WAZIRI MKENDA ATETA NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI DK.DONALD WRIGHT

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (Mb) akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright alipotembelea ofisi za Wizara jijini Dodoma

Waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (Mb) akimpa zawadi Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright mara baada ya kumaliza kikao cha pamoja kilichofanyika ofisi za Wizara jijini Dodoma

Waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright pamoja na ujumbe wake mara baada ya kumaliza kikao cha pamoja kilichofanyika ofisi za Wizara jijini Dodoma

……………………………………..

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Juni 7, 2022Jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright ambapo wamekubaliana kuendeleza ushirikiano katika elimu.

Baadhi ya maeneo waliyokubalina ni eneo la Sayansi, Teknolojia na Tiba ambapo kutakuwepo na fursa za wanafunzi kwenda kusoma nchini Marekani katika eneo hilo.

“Tunahitaji kufungua fursa nyingi zaidi za Watanzania kwenda kusoma katika vyuo vya Marekani katika maeneo ya sayansi, teknolojia na elimu ya tiba,” amesema Prof. Mkenda.

Katika hatua nyingine Prof. Mkenda amemueleza Balozi Wright kuwa kwa sasa kipaumbele kwenye Sekta ya Elimu ni kufanya mageuzi ya elimu ili elimu inayotolewa iweze kutoa ujuzi bila kuathiri ubora.

“Ni maelekezo ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha elimu inayotolewa inamuandaa mtoto kuwa na ujuzi, kwa hiyo kwa sasa tunapitia Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 na mabadiliko ya mitaala ii iweze kukidhi hayo,” amesema Prof. Mkenda.

Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright amesema nchi ya Marekani inafurahi kuwa na mashirikiano na nchi ya Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu lengo ni kuhakikisha ubora wa elimu kwa kila mtoto wa Kitanzania kwani elimu ndio nyenzo katika kufikia maisha bora.

About the author

mzalendoeditor