Featured Kitaifa

MILIONI 30 KUTATUA CHANGAMOTO ZAHANATI YA ILUNDA- SINGIDA

Written by mzalendoeditor

Muonekano wa matenki ya kuifadhi maji yaliyonunuliwa chini ya mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini unaotekelezwa katika Zahanati ya Ilunda Halmashauri ya Mkalama mkoani Singida

Mratibu wa mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini Ndg. Anyitike Mwakitalima akiwa amebeba mota iliyonunuliwa kwaajili yakupandishia maji kwenye matanki ya kuhifadhi maji katika Zahanati ya Ilunda halmashauri ya wilaya ya Mkalama Mkoani Singida.

imu ya Ufatiliaji wa mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini kutoka Wizara ya afya ikiongozwa na Ndg. Anyitike Mwakitalima wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Zahanati ya Ilunda katika halmashauri ya Mkalama mkoani Singida

Muonekano wa vyoo vinavyojengwa chini ya utekelezaji wa mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini katika zahanati ya Ilunda halmashauri ya Mkalama mkoani Singida

Mratibu wa mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini Ndg. Anyitike Mwakitalima akiongoza jopo la wataalamu kutoka wizara ya afya pamoja nauongozi wa Zahanati ya Ilunda kuhakiki vipimo vya mfumo wa maji taka katika Zahanati ya Ilunda Halmashauri ya Mkalama mkoani Singida

Mratibu wa mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini Ndg. Anyitike Mwakitalima akiongoza jopo la wataalamu kutoka wizara ya afya pamoja nauongozi wa Zahanati ya Ilunda kuhakiki vipimo vya mfumo wa maji taka katika Zahanati ya Ilunda Halmashauri ya Mkalama mkoani Singida

Muonekano wa tenki la kuifadhi maji linalojengwa chini ya mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini unaotekelezwa katika Zahanati ya Ilunda Halmashauri ya Mkalama mkoani Singida

……………………………………..

Na. WFA, MKALAMA -SINGIDA
Serikali kupitia wizara ya afya imetumia kiasi cha shilingi Milioni 30 kuboresha miundombinu ya mfumo wa maji safi na salama, kukarabati vyoo,wodi ya wazazi pamoja na sehemu za kunawia mikono katika Zahanati ya Ilunda iliyopo katika kata ya Ilunda halmashauri ya wilaya ya mkalama mkoani Singida.

Kauli hiyo imebainishwa na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Ilunda Dkt. John Sanga wakati alipotembelewa na Timu ya Ufatiliaji wa utekelezaji wa Mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini kutoka wizara ya Afya inayoongozwa na Ndg. Anyitike Mwakitalima.

Dkt. Sanga ameeleza kuwa kupitia Mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini utasaidia kupunguza magonjwa ya milipuko yatokanayo na kutokuwa na miundombinu Rafiki ya ufasi wa mazingira katika zahanati hiyo na jamii inayozunguka maeneo hayo.

“Mpaka sasa utekelezaji wa Mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini katika Zahanati yetu ya Ilunda tumefikia asilimia 60 na tunatarajia kukamilisha mradi huu ifikapo 30 Juni, Mwaka huu”, amesema Dkt. Sanga

Dkt. Sanga ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha katika kuboresha miundombinu mbalimbali katika zahanati hiyo ili kuleta ufanisi wa utoaji huduma bora katika mazingira rafiki na kuleta tija kwa wananchi wa kata ya Ilunda na maeneo jirani ya kata hiyo.

Kwa upande wake mwakilishi wa wananchi wa kata ya Ilunda Mzee Jonas Obadia, ameishukuru wizara ya afya chini ya uongozi makini wa Waziri Ummy Mwalimu kwa kuwa na timu imara na makini katika kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini.

“Kwa ufatiliaji huu timu kutoka wizara ya afya chini ya Mratibu wa mradi wa Huduma Endelevu za Maji na Usafi wa Mazingira vijijini Ndg. Anyitike Mwakitalima inaonyesha ni namna gani inajali na kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati, kwa viwango bora vinavyo hitajika na kuleta tija kwa wananchi wakata ya Ilunda ili kutatua changamoto ya maji katika zahanati hii”, ameeleza Mzee Obadia.

About the author

mzalendoeditor