Featured Kitaifa

MAGANGA ATAKA SOKO LA MAJENGO KUTUMIA VIFAA VYA KUKUSANYIA TAKA

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akisikiliza maelezo kuhusu usimamizi wa soko la Majengo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro wakati wa ziara ya kikazi leo Mei 30, 2022 kwa ajili ya kujionea jitihada za wadau katika usafi wa mazingira ambayo ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Kitaifa.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga wakia katika ya kikazi leo Mei 30, 2022 kwa ajili ya kujionea jitihada za wadau katika usafi wa mazingira ambayo ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Kitaifa.

…………………………………………..

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga ameelekeza uongozi wa soko la Majengo jijini Dodoma kuhakikisha wanakuwa na vifaa vya kukusanyia taka ngumu ili kuwe na utaratibu mzuri na ziweze kutenganishwa.
Amesema hayo leo Mei 30, 2022 wakati wa ziara ya kikazi kwa ajili ya kujionea jitihada za wadau katika usafi wa mazingira ambayo ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Kitaifa.
Bi. Maganga aliwataka wafanyabiashara hapo kuzingatia usafi wa mazingira hatua itakayosaidia kulinda afya za wananchi wanaofika kununua bidhaa za chakula sokoni hapo.
Alisema pamoja na soko hilo kuwa dogo na kusababisha watumiaji kubanana lakini maeneo ya kufanyia biashara yamepangwa vizuri na kutoa rai kwa uongozi wa soko kuifanyia kazi changamoto hiyo.
“Nisisitize kuwa usafi wa mazingira ni endelevu, utunzaji wa mazingira ni endelevu na awiki hii tunafana maadhimisho kujikumbusha kwa hiyo tunawakaribisha mshiriki nasi katika maadhimisho haya,” alisema.
Pia Katibu Mkuu Maganga aliwakumbusha wananchi kujitokeza kushiriki katika zoezi la Sensa ifikapo Agosti 2022 ili kuhesabiwa na kuweza kuingiza katika kumbukumbu.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI Bw. Ramadhan Kailima alitoa wito kwa uongozi wa soko kuwa na utaratibu wa kufanya vikao vyenye ajenda ya kujadili mikakati ya kutunza mazingira angalau mara moja kwa mwezi au miezi mitatu.
Pia Kailima aliwashauri kugawa maeneo ya soko ili kurahisisha usimamizi wa usafi kwa kutambua nani anasimamia eneo gani hatua itakayosaidia kuboresha mazingira ya soko hilo.

About the author

mzalendoeditor