YANGA imetinga Fainali ya Kombe la FA baada ya kuichapa na kuivua ubingwa Simba kwa kuichapa bao 1_0 Mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Shujaa wa Yanga ni Kiungo Mshambuliaji Fei Toto dakika ya 25 akifunga bao kwa shuti nzuri lililomshinda mlinda mlango wa Simba Ben Kakolonya.
Kwa ushindi huo Yanga wametinga Fainali na wanamsubiri kati ya Azam FC au Coastal Union ambao wanacheza kesho mechi itakayopigwa jijini Arusha.