Naibu katibu mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii Juma Mkomi akiongea katika hafla ya uvishwaji wa vyeo kwa makamisha wasaidizi wa uhifadhi wa shirika la hifadhi Tanzania (TANAPA).
Kamishna wa uhifadhi Tanzania William Mwakilema akiongea katika hafla ya uvishwaji wa vyeo kwa makamisha wasaidizi wa uhifadhi katika makao makuu ya shirika hilo mkoani Arusha.
Makamishna wasaidizi wakivishwa vyeo pamoja na kuapa katika hafla ya iliyofanyika makao makuu ya shirika la hifadhi Tanzania (TANAPA) jijini Arusha.
Makamishna, maofisa na maaskari wa shirika la hifadhi Tanzania waliohudhuria katika hafla hiyo.
Picha ya pamoja ya naibu katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii pamoja na makamisha wa shirika la hifadhi Tanzania (TANAPA)
……………………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Juma Mkomi amewataka makamisha wa shirika la hifadhi Tanzania (TANAPA) kuwa waadilifu kwenye kazi zao kwani uadilifu ni kitu cha msingi katika kulinda hifadhi.
Mkomi alitoa rai hiyo katika hafla ya uvishwaji wa vyeo kwa makamisha wasaidizi wa uhifadhi wa shirika hilo ambapo alisema kuwa lazima wawe waadilifu kwenye kulinda hifadhi, rasilimali na katika namna ya kuwasimamia wenzao.
“Niwaombe suala la uadilifu kuwa kipaumbele lakini ili kuwa na ulinzi endelevu katika maeneo yetu kuna kitu kinaitwa CSR, tafuteni namna nzuri ambayo wananchi wataweza kushiriki vya kutosha katika kusema ni namna gani au mradi gani wangeipenda na hii itasaidia kuhakikisha miradi hiyo inawagusa lakini watathamini kwa namna moja au nyingine,” Alisema Mkomi.
Aidha alifafanua kuwa kupitia CSR wanaweza wakasaidia na wanachi kujifunza namna ya uhifadhi kwasababu wataona tija ya hicho kinachofanyika pamoja na kuendelea kuuimba wimbo wa wizara wa wageni wakuja kwa vitendo kwa kuhakikisha kwamba wageni wanaendelea kuja na kwa kufanya hivyo Royor Tour itakuwa naaana na tija kubwa kwao.
Alisema wanahifadhi ili kulinda rasilimali hizo ziendelee kuwepo miaka na miaka ili kuongeza kipato cha nchi hivyo jambo la msingi ili Royor Tour iweze kufanikiwa na kukamilisha yale iliyoyalenga, cha kwanza ni uhifadhi wa maeneo yao kwani wasipo hifadhi vivutio vitapoteza ubora.
Kwa upande wake kamishnaTanzania William Mwakilema aliwaelekeza kupitia majukumu yao kuwa makini kwani watapaswa kuyatekeleza ipasavyo ambapo atumaini kuwa watatumia vipawa vyao, vipaji, uzoefu,elimu na busara katika kuwaongoza watumishi watakao kuwa chini yao.
“ Katika maeneo yenu ya kazi mnapaswa kuwa viongozi kwa kuonyesha njia, nendeni mkawaunganishea maafisa na askari mtakaowasimamia ili kutimiza malengo ya shirika na nchi kwa ujumla,” Alisema Mwakilema.
Aidha aliwataka maofisa na maaskari wote kutoa ushirikiano wa kutosha ili makamishna hao wasaidizi wa uhifadhi walio teuliwa waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo lakini pia wawendelee kujituma na kutekeleza wajibu wao pamoja na kuimarisha nidhamu ndani ya jeshi, nidhamu binafsi na nidhamu kwa wengine.
“Nidhamu ndio msingi wa jeshi lolote ili kuimarisha utendaji kazi lakini viongozi wote ambao mmepata uteuzi ama kubadilishiwa vituo vya kazi hakikisheni mnakamilisha zoezi la makabidhiano ya ofisi katika kipindi kifupi ili kila mmoja aweze kuripiti katika kituo chale cha kazi ili kuendelea na yaliyo mbele yetu kwa kuzingatia kuwa tunaelekea katika kipindi Cha mwisho wa kufunga mwaka wa fedha,”Aliagiza.