Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (Mb) akiwa kwenye Taasisi inayojishughulisha na Teknolojia na ubunifu wa mazao yatokanayo na ngozi ya Chuo Kikuu cha Northampton nchini Uingereza
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi William Lohay na Azaria Chongeri ambao ni watumishi kutoka DIT kampasi ya Mwanza wanaosoma kwenye Taasisi inayojishughulisha na Teknolojia na ubunifu wa mazao yatokanayo na ngozi ya Chuo Kikuu cha Northampton nchini Uingereza
………………………………………..
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof. Adolf Mdenda (Mb) leo Mei 25, 2022 ametembelea Taasisi inayojishughulisha Teknolojia na ubunifu wa mazao yatokanayo na ngozi ya Chuo Kikuu cha Northampton nchini Uingereza.
Akiwa katika Chuo hicho Waziri Mkenda amefanya mazungumzo na uongozi wa wa Juu wa Chuo hicho na kukubaliana kuwa na Makubaliano maalum (MoU) ya kuwezesha kuanza kubadilishana uzoefu watumishi wa Chuo hicho na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Chuo Kikuu Sokoine cha Kilimo (SUA) pamoja na kuanza kutoa ufadhili (scholarship) kwa wanafunzi wa kitanzania katika eneo hilo.
Aidha Prof. MKenda amefurahi kukutana na wanachuo wawili wa kitanzania William Lohay na Azaria Chongeri wanaosoma chuoni hapo ambao ni watumishi wa DIT kampasi ya Mwanza. DIT kampasi ya Mwanza ni mahsusi kwa eneo la tenolojia ya mazao ya ngozi .
Waziri Mkenda yuko nchini uingezera ambapo anahudhuria kongamano lwa Mwaka la kimataifa la Elimu. *World Education Forum 2022.*