Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza katika siku ya pili ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) tarehe 25 Mei, 2022 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Accra, Ghana mara baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) kutokana na Mafanikio yake kwenye Ujenzi wa Barabara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 kutoka kwa Makamu wa Rais wa Sekta Binafsi, Miundombinu na Viwanda kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Solomon Quaynor kwa niaba ya Rais wa Benki hiyo Dkt. Akinumwi Adesina. Hafla ya Utoaji wa Tuzo hiyo imefanyika kwenye siku ya pili ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa AfDB, Accra nchini Ghana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) kutokana na mafanikio kwenye Ujenzi wa Barabara, mara baada ya kukabidhiwa Tuzo hiyo na Makamu wa Rais wa Sekta Binafsi, Miundombinu na Viwanda katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Solomon Quaynor tarehe 25 Mei 20220 Accra nchini Ghana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Sekta Binafsi, Miundombinu na Viwanda katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Solomon Quaynor pamoja na viongozi mbalimbali wa Benki hiyo mara baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) kutokana na mafanikio kwenye Ujenzi wa Barabara.