Featured Kitaifa

KATIBU MKUU MADINI AFUNGA JUKWAA LA KWANZA LA UTEKELEZAJI WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI JIJINI MWANZA

Written by mzalendoeditor

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Madini, Adolf Ndunguru

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Madini, Adolf Ndunguru leo tarehe 22 Mei, 2022
amefunga Jukwaa la Kwanza la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania
Katika Sekta ya Madini lililoanza tangu tarehe 20 Mei 2022 jijini
Mwanza.

Jukwaa hilo
lililoambatana na maonesho lilishirikisha wadau wa madini wakiwa ni
pamoja na wachimbaji wa madini, watoa huduma kwenye shughuli za
uchimbaji wa madini, mabenki, na watendaji kutoka Taasisi zilizopo chini
ya Wizara ya Madini.
Akizungumza
kwenye ufungaji wa jukwaa hilo Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adolf
Ndunguru amesema kuwa Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini imeandaa
jukwaa kwa lengo la kuhakikisha watanzania wanabaini fursa zilizopo na
kushiriki kikamilifu kwenye Sekta ya Madini.
Amesema
kuwa Wizara ya Madini itaendelea kuhakikisha watanzania wananufaika na
Sekta ya Madini kupitia ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya
madini pamoja na kutatua changamoto mbalimbali.
Aidha,
amewataka wadau wa madini kushiriki katika zoezi la sensa
linalotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu ili kuiwezesha Serikali
kuweka mipango mbalimbali ya maendeleo.
_Wakati
huohuo,_ Ndunguru ametoa tuzo na vyeti kwa wadhamini wa Jukwaa hilo
wakiwa ni pamoja na  Equity Bank (Tanzania) Limited, CMS (Tanzania)
Limited, Twiga Minerals Corporation Limited na BR Drilling Limited.
Wengine
ni pamoja na Tansec Limited, Boart Longyear (Tanzania) Limited, Geita
Gold Mining Limited, Williamson Diamonds Limited, Tembo Nickel
Corporation Limited, BG Umoja Services Limited, Epsom Limited,  African
Assay Laboratories, Tanga Cement Limited, Shanta Mining Co. Limited na
SGA Guards Tanzania Limited.
Akizungumza
kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Kamishna wa Tume ya Madini, Janet
Reuben Lekashingo sambamba na kushukuru kwa ushirikiano mkubwa
unaotolewa na Wizara ya Madini kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini
amewataka wananchi kuchangamkia fursa zilizopo kwenye Sekta ya Madini.
Naye
Kamishna wa Madini, Dkt. Abdulrahman Mwanga amesema kuwa jukwaa
limewapa mwanga wadau wengi wa madini kuhusu dhana nzima ya
ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini.
Aidha
amesema kuwa  jukwaa hilo limetumika kama njia mojawapo ya kujadili 
namna ya kuzitatua changamoto mbalimbali zinazoikumba Sekta ya Madini
hususan kwenye eneo la ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya
Madini.
Naye Mkuu wa
Wilaya ya Ukerewe, Kanali Dennis Mwila akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel ameipongeza Tume ya Madini kwa
kuandaa jukwaa la kizalendo lenye lengo la kuhakikisha watanzania
wanafahamu namna wanavyoweza kushiriki kwenye Sekta ya madini kupitia
utoaji wa huduma kwenye migodi ya madini.
Aidha, 
amewataka washiriki wa jukwaa hilo kuwa wazalendo kwenye utekelezaji wa
shughuli zao na kupata fursa zaidi kwenye migodi ya madini.

About the author

mzalendoeditor