Featured Kitaifa

BENKI YA NBC YAKUTANA NA WATEJA WAKE MKOANI MBEYA,YATAMBULISHA HUDUMA MPYA

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali wa Benki ya NBC, Bw  Mussa Mwinyidaho (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na wageni waalikwa akiwemo Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Masoko (TCCIA)  Mkoa wa Mbeya Bw Erick Sichinga (wa pili kushoto) wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo mwishoni mwa wiki kwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa jijini Mbeya ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo kupitia huduma yake ya NBC Biashara Club.

Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali wa Benki ya NBC, Bw  Mussa Mwinyidaho akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa jijini Mbeya ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo kupitia huduma yake ya NBC Biashara Club.

Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Masoko (TCCIA)  Mkoa wa Mbeya Bw Erick Sichinga akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa jijini Mbeya ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo kupitia huduma yake ya NBC Biashara Club.

Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbeya Bi Asia Mselemu akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa jijini Mbeya ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo kupitia huduma yake ya NBC Biashara Club.

Meneja Bidhaa na Huduma za Kibenki wa Benki ya NBC, Jonathan Bitababaje akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa jijini Mbeya ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo kupitia huduma yake ya NBC Biashara Club.

Sehemu wa wageni waliohudhuria hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa jijini Mbeya ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo kupitia huduma yake ya NBC Biashara Club.

Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali wa Benki ya NBC, Bw  Mussa Mwinyidaho (katikati walioketo) pamoja na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Masoko (TCCIA)  Mkoa wa Mbeya Bw Erick Sichinga (wa pili kulia walioketi) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo mwishoni mwa wiki kwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa jijini Mbeya ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo kupitia huduma yake ya NBC Biashara Club.

………………………………………..

Na.Mwandishi Wetu-Mbeya

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekutana na wateja wake wadogo na wakubwa wa jijini Mbeya ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo sambamba na kuwaelimisha wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Benki hiyo pia ilitumia fursa hiyo kujadili na wateja hao namna inavyoweza kuboresha huduma zake kulingana na mahitaji yao.

Akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo mwishoni mwa wiki kupitia huduma yake ya NBC Biashara Club, Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali wa Benki hiyo Bw  Mussa Mwinyidaho alisema benki ya NBC imedhamiria kuboresha huduma zaidi ili wateja wake waendelee kufurahia huduma zilizorahisishwa zaidi ili kuendana na matakwa ya shughuli zao ili waweze kukuza biashara zao.

“Kupitia NBC Biashara Club tumekuwa na mkakati mpana wa kuwainua wajasiriamali kwa kuwajengea uwezo wa kibiashara kupitia semina za mafunzo, kuwasogezea huduma za kibenki, kuwajengea mitandao ya kibiashara pamoja na kuwapa mbinu za kurasimisha biashara zao ili waweze kukopesheka. Mpango huu umekuwa na tija si tu kwa wateja wetu bali pia hata sisi kama benki tumeweza kupata mrejesho uliotuwezesha kuboresha huduma zetu kwa ajili yao,’’ alisema.

Alisema kupitia klabu hiyo, benki hiyo imeweza kutangaza huduma mpya kwa ajili ya wajasiriamali ikiwemo huduma ya ‘Commercial Property Financing’ inayowawezesha wajasiriamali wenye majengo ya biashara kupata mikopo yenye marejesho nafuu sambamba na huduma ya ‘Commercial Asset Financing’ inayowawezesha wajasiriamali hao kukopa mitambo kwa ajili ya biashara na shughuli za ukandarasi.

“Pia kupitia tukio hili la leo wateja wetu mkoani Mbeya watapata fursa ya kufahamu huduma zetu za mikopo bila dhamana  ikiwepo huduma ya ‘Distributor financing’ inayowawezesha wajasiriamali kupata mikopo ya kusambaza bidhaa zao  bila dhamana pamoja na huduma ya ‘Purchasing Order Financing’ inayowawezesha wajasiriamali kupata mikopo kwa kutumia Hati ya manunuzi yaani LPO ,’’ alisema.

Zaidi, Mwinyidahao alibainisha kuwa  kupitia huduma ya NBC Biashara Club benki hiyo imeweza kuwakutanisha wanachama wa klabu hiyo na watoa huduma mbali mbali katika sekta ya biashara zikiwemo taasisi za serikali kama TRA, BRELA, TBS na nyingine nyingi ili kujadili na kutatua changamoto na kupata mafunzo zaidi kwenye masuala muhimu ikiwemo elimu kuhusu kodi.

Akizungumza kwa niaba ya wateja hao, Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Masoko (TCCIA)  Mkoa wa Mbeya Bw Erick Sichinga, mbali na kuonesha kuunga mkono mapinduzi ya huduma za kibenki kupitia benki ya NBC alisema wafanyabiashara mkoani humo wameridhishwa kwa kiasi kikubwa na mchango wa huduma ya NBC Biashara Club kwa kuwa kupitia klabu hiyo wameweza kupata mafunzo ya kibiashara sambamba na kuelimishwa kuhusu fursa mpya za masoko na biashara.

 “Suala la benki kubuni huduma mpya ni jambo moja ila kuhakikisha huduma hiyo inaeleweka na inatumiwa vema na walengwa ambao ni sisi wateja nalo jambo zuri zaidi. Tunashukuru sana NBC kwa kuwa si tu wanabuni huduma zinazotugusa bali pia wamekuwa wakihakikisha tunapata uelewa wa kutosha kuhusu huduma hizo kupitia huduma hii ya NBC Biashara Club.’’ Alisema

Alisema hatua hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa wafanyabiashara hao kwa kuwa imekuwa ikiwawezesha kufanya uamuzi sahihi kuhusu huduma mahususi zinazoendana na aina ya biashara zao,’’ alisema.

About the author

mzalendoeditor