Featured Kitaifa

SOMO LA TEHEMA LIMERAHISISHA UTOAJI WA ELIMU – MASHULENI KUPITIA MEWAKA

Written by mzalendoeditor

Asila Twaha, Urambo

Serikali inatambua umuhimu wa somo la TEHAMA katika Sekta ya Elimu hasa kwa kutumia kama nyenzo ya kuongeza maarifa na ujuzi katika ufundishaji na ujifunzaji ndio mana mafunzo mbalimbali kwa sasa yanatolewa kwa njia ya masafa ili walimu waweze kuendana na wakati wa sasa.

Hayo amesema Mwezeshaji wa Mafunzo Endelevu Kazini (MEWAKA) Bi. Paula Soko wakati wa mafunzo yanayoendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo walimu na kujua lengo la mafunzo hayo.

Soko amesema, pamoja na upitishwaji katika miongozo minne ambapo ni miongozo ya tathmini ya mahitaji ya walimu, uanzishwaji wa vituo vya MEWAKA, utekelezaji katika ngazi za shule na vituo vya walimu na usimamizi wa MEWAKA, somo la TEHAMA kwa walimu limefungua ufahamu mkubwa wa kuweza kupata njia za ujifunzaji na ufundishaji kwa watoto wetu.

Vilevile Soko ameeleza katika kujua miongozo hiyo lakini pia walipitishwa katika moduli ambapo wamezipata katika mfumo wa Kieletroniki kupitia TEHAMA walimu wameweza kusoma kwa vitendo kwa kuweza kutumia simu janja na kopyuta kwa kuweza kupata “materials” zilizoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania.

“Ni toe wito walimu wenzangu dunia ya ya sasa inataka tufahamu vitu vingi nafahamu wengi tunatumia simu janja tuzitumie vizuri kwa faida tutakuwa na uwezo wa kujiendeleza wenyewe tukiwa kazini tutapata mambo mengi katika kufanya kazi zetu” amesema Soko

Naye Mratibu wa Mafunzo Mkoa wa Tabora Bw. Inyasi Kanisi ameishukuru Serikali kwa kwa mafunzo hayo kuendelea Mkoa huo amesema Halmashauri tano zinaendelea na mafunzo Urambo, Uyui, Igunga, Kaliua na Sikonge aidha, ameeleza jumla ya washiriki 1157 wamepata mafunzo na anaamini kwa idadi hiyo wataenda kuwa mfano mzuri kwa wengine kwa kuwaelekeza.

Mshiriki wa Mafunzo ya MEWAKA Mwl. Baraka Kisesebe amesema mpango uliokuja wa kuwezesha walimu hasa kutumia ufundishaji wa mtandao utawasaidia kupata vitabu vya kufundishia na mbali ya vitabu wataweza kujiendeleza kielimu hata kama wapo mbali wataweza kusoma kwa kutumia njia ya masafa.

“ Tunaiomba Serikali iendelee kuwekeza katika miundombinu ya elimu na upatikanaji wa mawasiliano sehemu ambazo hazina ili walimu tuwe na urahisi wa kuweza kupata mawasiliano sababu mbali ya kuwa na simu janja lakini inatakiwa iwe na uwezo wa kupata mtandao”

About the author

mzalendoeditor