Featured Kitaifa

WAZIRI UMMY AZINDUA AWAMU YA PILI YA KAMPENI YA CHANJO YA MATONE YA POLIO NCHINI

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutoa chanjo ya matone ya Polio uliofanyika leo Mei 18,2022 kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Staslaus Nyongo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutoa chanjo ya matone ya Polio uliofanyika leo Mei 18,2022 kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Tumaini Macha,akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutoa chanjo ya matone ya Polio uliofanyika leo Mei 18,2022 kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kuleta watoto wao kupata chanjo ya matone ya polio leo jijini Dodoma katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya matone ya polio

Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Dodoma wakifatilia kwa makini uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya matone ya polio leo jijini Dodoma

Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Dodoma wakifatilia uzinduzi wa Kampeni ya Chanjo ya matone ya polio jijini Dodoma

Mmoja wa Mashuhuda ambaye amewahi kuugua Ugonjwa waPolio Issa Ibrahimu akiwa katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya matone ya polio iliyofanyika leo jijini Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu  katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya matone ya polio iliyofanyika Jijini Dodoma

Moja ya Kikundi cha Burudani kutoka Dodoma wakitoa burudani kwenye hafla ya uzinduzi wa chanjo ya matone ya polio leo Jijini Dodoma

Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu,akiwa na viongozi wakionyesha Mwongozi mara baada ya kuzindua kampeni ya kutoa chanjo ya matone ya Polio uliofanyika leo Mei 18,2022 kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akimpatia mmoja wa watoto walioletwa kupata chanjo ya matone ya polio kama ishara ya uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya matone ya polio jijini Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka akimpatia mtoto chanjo ya matone ya polio mmoja wa watoto waliojitokeza kupata chanjo hiyo kama ishara ya uzinduzi wa kampeni ya chanjo hiyo katika mkoa wa Dodoma

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na wazazi waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya matone ya polio leo Mei 18,2022 jijini Dodoma

…………………………………………
Na.Alex Sonna, Dodoma
Serikali kupitia wizara ya Afya imesema Jumla ya Watoto 10,295,316 wanatarajiwa kufikiwa kwa Tanzania Bara na Zanzibar kwa awamu hii ya pili ya kampeni ya Chanjo ya Matone ya Polio kwa Watoto.

Kauli hiyo imetolewa Leo Mei 18,2022 jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu katika uzinduzi wa kampeni ya kutoa chanjo ya matone ya Polio kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma ambapo awamu ya kwanza ilifanyika katika mikoa ya Njombe,Mbeya, Ruvuma na Songwe na waliwafikia watoto 1,138,949 kati ya 983,542 waliokusudiwa.

Waziri Ummy amesema lengo la kampeni hiyo ya utoaji wa chanjo ya matone ya Polio kwa watoto wote wenye umri wa miaka mitano inayofanyika nchi nzima kwa siku nne ni kuongeza kinga mwilini kwa watoto na hivyo kuzuia kuenea kwa maambukizi ya Kirusi cha Polio kilichoripotiwa kuwepo nchi jirani ya Malawi.

“Kampeni hii itakua ni ya siku nne na itafanyika kwenye vituo vya huduma za afya pamoja na kuwafuata watoto mahali popote walipo ili kuwapatia huduma hii ya chanjo yam atone ya polio”, ameeleza Waziri Ummy.

Hata hivyo Waziri Ummy ametoa wito kwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI kusimamia matumizi sahii ya fedha za chanjo zilizotolewa kwenye halmashauri zote nchini ili kuleta ufanisi katika kampeni hii.

Vile vile Waziri Ummy amewataka wananchi kutokuamini taarifa za upotoshaji zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu chanjo nchini.

“Hatutakubali kuona watu wachache kwa maslahi yao wakiiweka Tanzania hatarini kwa ugonjwa wa Polio,Vyombo vya usalama wachukulieni hatua wale wote wanaosambaza taarifa za uzushi na kupotosha jamii kuhusu chanjo, chanjo hizi ni salama”, amesisitiza Waziri Ummy

About the author

mzalendoeditor