Kocha wa Mbeya Kwanza, Mbwana Makata na Meneja David Naftali wamefungiwa kwa kipindi cha miaka mitano (5) kila mmoja kwa kosa la kushawishi/kuamuru wachezaji wasiingie uwanjani kuanza mchezo kati ya Namungo dhidi ya Mbeya Kwanza , tukio lililosababisha mchezo usifanyike na kuchafua taswira ya Ligi ikiwemo kusababisha hasara kwa wadhamini wa Ligi.


Mechi ya hiyo haikufanyika kwasababu Mbeya Kwanza iligoma kucheza kwa kile walichoeleza kuwa ni kutokamilika kwa moja ya taratibu za maandalizi ya mchezo (uwepo wa gari la kubebea wangonjwa kwenye uwanja wa Ilulu, Lindi kabla ya kuanza mchezo huo).

Baada ya gari ya kubebea wagonjwa kuchelewa kufika na wao wakisema kikanuni ni dakika 15 zinatakiwa kusubiri na TPLB imesema kwa mujibu wa kanuni ni dakika 30.

Previous articleKATIBU MKUU CCM CHONGOLO ATETA NA KATIBU MKUU WA CNDD FDD JIJINI DAR ES SALAAM
Next articleSPIKA DKT. TULIA ACKSON AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI BUNGENI JIJINI DODOMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here