Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akisalimiana na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Donald Bombo alipowasili katika kikao kazi cha wadau wa NGOs kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kilichofanyika Mei 14, 2022 jijini Mbeya.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akizungumza katika kikao cha wadau wa NGOs kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kilichofanyika Mei 14, 2022 jijini Mbeya.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usajili na Uratibu wa NGOs kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Grace Mbwilo akitoa maelezo ya Awali katika kikao cha wadau wa NGOs kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ukusanyaji maoni juu ya Mkakati wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kilichofanyika Mei 14, 2022 jijini Mbeya.
Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha kuratibu ukusanyaji maoni juu ya Mkakati wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nensia Mahenge akieleza namna kikosi kazi hicho kinavyoendelea kukusanya maoni hayo katika kikao cha wadau wa NGOs kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kilichofanyika Mei 14, 2022 jijini Mbeya.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kikao cha wadau wa NGOs nchini kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kilicholenga ukusanyaji wa maonj kuhusu Mkakati wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kilichofanyika Mei 14, 2022 jijini Mbeya.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM
……………………………………..
Na WMJJWM- Mbeya
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju amekitaka Kikosi Kazi cha kuratibu ukusanyaji maoni kuhusu Mkakati wa Uendelevu wa NGOs kushirikiana na wadau nje ya Sekta hiyo kupata maoni yatakayosaidia kuwa na Mkakati wenye tija kwa maendeleo ya NGOs.
Mpanju ameyasema hayo Mei 14, 2022 jijini Mbeya wakati akifungua kikao cha wadau wa NGOs kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kilicholenga ukusanyaji maoni juu ya Mkakati wa Uendelevu wa NGOs nchini.
Aliongeza kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha NGOs zinakuwa na mazingira mazuri ya kushiriki kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhudumua jamii na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mpanju alisema ili kuwa na mkakati wenye tija ni muhimu wadau wote wakashirikishwa katika kutoa maoni yao ili kuwa na uwanda wa mawazo na kuwa na Mkakati shirikishi.
“Pamoja na yote mtakayoyatekeleza hakikisheni ili tuwe na mpango kazi unaoakisi uhalisia mkutane pia na wadau wa ambao wapo nje ya Sekta yenu ya NGOs “alisema Mpanju
Mpanju alisema lengo la mkakati huo wa kitaifa ni kuwa na dira ya namna ya NGOs kuweza kujitegemea na kuwa na uendelevu wa shughuli wanazofanya hivyo amewataka Wasajili wasaidizi wa Mikoa na Wilaya ambao ni Maafisa Maendeleo ya Jamii kushiriki katika kuhakikisha NGOs hazilundikani katika eneo moja zikitoa huduma zinazofanana kwa watu wa eneo moja.
“Zoezi hili ni kwa ajili yenu kupata fursa ya kutoa maoni kwa niaba ya NGOs na kwa maslahi ya wananchi mnao wahudumia nyie ni wadau muhimu sana mnaofanya kazi njema, kazi ya kutukuka, kuleta ukombozi, elimu na kuwainua wananchi ambao ni wanufaika kupitia kazi zenu” alisema Mpanju.
Aidha alibainisha kuwa Serikali inatambua mchango wa NGOs kwani sekta hiyo imesaidia kuongeza ajira kwa wananchi na pia kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na ukatili dhidi ya wanawake,watoto na kiketabusawa wa Kijinsia katika jamii.
Wakati huo huo Naibu Katibu Mkuu Amon Mpanju ametumua fursa hiyo kuhumiza familia kuwa na Utamaduni wa kuzungumza na kuzingatia malezi na makuzi bora ya Watoto katika jamii kuelekea Siku ya Kimataifa ya Familia inayofanyika kila Mei 15 na .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha kuratibu ukusanyaji maoni juu ya Mkakati wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nensia Mahenge alisema Mkakati huo wa Uendelevu wa Mashirika ya itasaidia Mashirika hayo kuweka kujiendesha na kutekeleza majukumu yao hata kusipokuwepo na ufadhili kutoka kwa wadau wa maendeleo.
“Tusikie maoni mapendekezo mawazo ya wadau wote kuhusu kuendelea kutoa huduma kwa jamii bila kuathiriwa na sababu mbalimbali ikiwemo ufadhili wa nje, tumeshuhudia wakati wa majanga mbalimbali, baadhi ya Mashirika kushindwa kujiendesha” alisisitiza Nensia.
Naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Donald Bombo alisema Mkoa wa Mbeya unashirikia karibu na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kutekeleza miradi mbalimbali na huduma kwa wananchi hasa katika maeneo ya vijijini.
Nao baadhi ya wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini walisema Mkakati huo utasaidia NGOs kuwa na uwezo wa kuendelea kutekeleza majukumu yao kupitia miradi na utoaji wa huduma kwa wananchi hivyo kupunguza utegemezi kutoka kwa wafadhili.