Featured Kitaifa

MAJALIWA ATETA NA BALOZI WA KOREA YA KUSINI NCHINI KUHUSU UJENZI WA MELI YA MV MWANZA HAPA KAZI TU

Written by mzalendoeditor

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao kati yake na Balozi wa Korea Kusini Nchini, Kim Sun Pyo (kulia)  kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya  Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Mei 14, 2021. Wengine walioshiriki katika mazungumzo hayo ni  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk  N. Mbarouk, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,  Fred Makibete, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  Gas Entec Tanzania ambayo inatekeleza ujenzi wa meli ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu, Dongmyung Kwak, Bw. Philemon Bagambilana, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli,  Kanali Samweli Mahirane, Kamishina  wa Uhamiaji , Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka nchini    na Balozi Caesar Waitara ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Korea  ya Kusini nchini,  Kim Sun Pyo baada ya mazungumzo kati yao  kwenye ukumbi wa Ofisi  Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Mei 14, 2022. Wengine walioshiriki katika mazungumzo hayo ni  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk  N. Mbarouk, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,  Fred Makibete, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  Gas Entec Tanzania ambayo inatekeleza ujenzi wa meli ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu, Dongmyung Kwak, Bw. Philemon Bagambilana, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli,  Kanali Samweli Mahirane, Kamishina  wa Uhamiaji , Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka nchini    na Balozi Caesar Waitara ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki.Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Balozi wa Korea  ya Kusini nchini,  Kim Sun Pyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo kati yao  kwenye ukumbi wa Ofisi  Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Mei 14, 2022. Wengine pichani  ni  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk  N. Mbarouk (kulia kwa Waziri Mkuu) , Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,  Fred Makibete (kulia) , Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  Gas Entec Tanzania ambayo inatekeleza ujenzi wa meli ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu, Dong Myung Kwak (aliyesimama nyuma katikati), Bw. Philemon Bagambilana, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (nyuma kushoto) ,  Kanali Samweli Mahirane, Kamishina  wa Uhamiaji , Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka nchini  (nyuma kulia)   na Balozi Caesar Waitara ambale ni Mkurugenzi wa idara ya Asia na Australia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki (kushoto).

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

………………………………………………

SERIKALI imeuelekeza uongozi wa  Kampuni ya  Gas Entec Tanzania ambayo inajenga meli mpya ya MV Mwanza Hapa Kazi  Tu kuzingatia makubaliano  yote   yaliyomo kwenye mkataba wa ujenzi wa meli hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa  Kassim Majaliwa leo Mei 14, 2022  katika kikao kati yake na Balozi wa Korea ya Kusini nchini, Kim Sun Pyo kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam.   

Katika Kikao hicho ambacho kilihudhuriwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Gas Entec Tanzania  Bw. Kwak ambaye alikiri  mapungufu katika utekelezaji wa mradi huo na aliahidi kuwa kampuni yake itaongeza kasi ya ujenzi ili ukamilike kwa wakati na meli hiyo iwezo kuwahudumia wananchi kama ilivyokusudiwa.

Pia, Mheshimiwa Waziri Mkuu ameelekeza  kuwa  watalaamu wa Kampuni ya  Gas Entec Tanzania warejeshewe Pasi zao za kusafiria ambazo zilizuiwa na s

Serikali  kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika mwenendo wa ujenzi wa meli hiyo.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Mbarouk Mbarouk na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Fred Mwakibete. 

Wengine ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa  Kampuni ya Huduma za meli, Philemon Bagambilana  na Kanali Samwel Mahirane ambaye ni Kamishina wa Uhamiaji, Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka nchini.

About the author

mzalendoeditor