Featured Kitaifa

ATCL KUANZISHA SAFARI ZAKE TANGA BAADA YA UPANUZI KUKAMILIKA

Written by mzalendoeditor

MKurugenzi Mtendaji Mkuu wa
Shirika hilo Ladislaus Matindi akizungumza wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua uwanja wa
ndege wa Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza wakati wa ziara hiyo

Meneja wa Uwanja wa Ndege Mkoani Tanga Mussa Mcholwa akizungumza wakati wa ziara hiyo

Mkurugenzi
Mtendaji Mkuu wa
Shirika hilo Ladislaus Matindi katika akitembelea uwanja huo kulia ni
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima na kushoto ni Meneja wa uwanja wa
Ndege Tanga

Mussa Mcholwa

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima kulia akimuonyesha kitu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa
Shirika hilo Ladislaus Matindi wakati wa ziara yake

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.

 

SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL)
limesema lipo tayari kuanzisha safari zake za Tanga mara baada ya mpango wa
upanuzi wa uwanja wa Ndege Tanza utakapokamilika

 

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa
Shirika hilo Ladislaus Matindi wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua uwanja wa
ndege wa Tanga ambapo alisema mkoa huo ni moja ya sehemu ambayo wamekuwa
wakihudumia kwa miaka iliyopita.

 

Alisema lakini teknolojia ya viwanja
na matakwa kubadilika hivyo kwa ndege waliyonayo hivi sasa ya kiwanja kuwa
kifupi hakiwezi kuhimili uwezo wa ndege walizonazo. 

 

Aidha alisema upanuzi wa uwanja huo
utahusisha njia ya kurukia ndege( runway)ili uweze kuwa na uwezo wa kuhudumia
ndege na sababu ipo kubwa tuu kwa kuwa mzunguko hasa wa kibiashara Tanga ni mkubwa
hivyo suala hilo serikali imeliona na kuanza kulifanyia kazi.

 

Awali akizungumza wakati wa ziara
hiyo,Meneja wa Uwanja wa Ndege Mkoani Tanga Mussa Mcholwa alisema upanuzi huo
wa uwanja utakapokamilika utasaidia kuongeza fursa za kibiashara na
kiuchumi. 

 

“Ndege kubwa saizi ya kati
zitatua mzunguko utaongezeka, sababu kama bombadier Q4100 inabeba abiria 80
kwahiyo mnaweza mkaona kutoka abiria 12 kwenye caravan mpaka abiria 80 hivyo
sisi kama Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania tutaongeza, mapato pindi
kiwanja hichi kitakapopanuliwa alibainisha,” Meneja huyo. 

 

Aidha alisema kwamba Serikali
inaangalia mpango wa namna ya upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Mkoani Tanga ili
kukiwezesha kuweza kuwa na  uwezo wa
kutumiwa na ndege kubwa za abiria. 

 

Hata hivyo alisema mpango wa
Serikali ni kukifanyia upanua kiwanja hicho kutoka mita 1250 zilizopo hivi
sasa hadi kufikia mita 1700 ambazo zitawezesha ndege kubwa kuweza kutua. 

 

 

Naye kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Tanga Adam Malima alisema Serikali inaangalia namna ya kuupanua uwanja huo ili
uweze kuhudumia ndege  kubwa kutoka
maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

 

Malima alisemaTanga ni moja ya mikoa
ya  kibiashara hususani kwa wasafiri wa
ndege kwani wapo watu wanaotamani kutoka Tanga kwenda kufanya shughuli zake
maeneo mengine na jioni kurejea. 

 

About the author

mzalendoeditor