Featured Kitaifa

SHEIKH MUSTAPHA:’TUSHIRIKIANE KATIKA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KIMAENDELEO’

Written by mzalendoeditor

Sheikh wa mkoa wa Dodoma, Alhaj Mustapha Rajabu Shaabani, akikagua ujenzi unaendelea wa msikiti na madrasa ya Masjid Muccadam ulipo chang’ombe jijini Dodoma

Sheikh wa mkoa wa Dodoma Alhaj Mustapha Rajabu Shaabani, akikagua madarasa ya wanafunzi katika msikiti wa Masjid Muhammad (Markaz) uliopo area a jijini Dodoma katika ziara maalum alioifanya ya ukaguzi wa misikiti na madrasa katika mtaa wa chang’ombe jijini Dodoma

Sheikh wa mkoa wa Dodoma Alhaj Mustapha Rajabu Shaabani, akiongozana na baadhi ya viongozi wa baraza lake katika ukaguzi wa mabweni ya wanafunzi wa madrasa katika msikiti wa ALMADRASATU SHAMSIYAH ISLAMIC CENTER, ulipo mji mwema jijini Dodoma na kikabidhi kiasi cha shilingi Laki Mbili kwaajili ya kumaliza unjezi wa mabweni hayo.

Sheikh wa mkoa wa Dodoma Alhaj Mustapha Rajabu Shaabani, akikagua ujenzi wa madrasa na mabweni ya wanafunzi katika ziara alioifanya hapo jana, katika mtaa wa chang’ombe jijini Dodoma.

Sheikh wa mkoa wa Dodoma Alhaj Mustapha Rajabu Shaabani, akikagua ujenzi unaoendelea katika msikiti wa MARKAZI CHANG’OMBE na aliweza kukabidhi kiasi cha Shilingi Laki Mbili kwaajili ya kuwezesha ujenzi kuendelea Aliya fanya hayo katika ziara maalum ya ukaguzi wa misikiti na madrasa katika mtaa wa chang’ombe jijini Dodoma

Sheikh wa mkoa wa Dodoma Alhaj Mustapha Rajabu Shaabani, akiongozana na baadhi ya viongozi wa baraza lake katika ukaguzi wa kiwanja cha mwalimu wa madrasa kikichopo mji mwema jijini Dodoma ukaguzi huo ulifanyika katika ziara maalum ya ukaguzi wa misikiti na madrasa katika mtaa wa chang’ombe jijini Dodoma

………………………………………………

Na Julius Natale, Dodoma.

SHEIKH  wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu Shabani, amewataka waumini wote  wa dini ya Kiislamu kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii zenye kuleta maendeleo bila kusahau shughuli  za ujenzi wa nyumba za ibada.

Sheikh Mustapha ameyasema hayo wakati alipokuwa akifanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa Madrasa pamoja na Misikiti inayojengwa katika Wilaya ya Dodoma Mjini kata ya Chang’ombe na Bonanza.

Aidha Sheikh Mustapha alisema kuwa ushirikiano ni miongoni mwa jambo muhimu katika kuendeleza maadili ya dini na kuimarisha maendeleo kwa waumini na wadau wanaojitokeza katika kuisaidia jamii.

Pia aliwashukuru viongozi mbalimbali wa dini, serikali na wadau kwa kuendelea kuchangia maendeleo ya kujengwa kwa misikiti inayopatikana katika mikoa mbalimbali nchini.

“Niwashukuruni viongozi na waumini Mwenyezi Mungu awabariki kwa umoja wenu lakini zaidi ni Dua zenu mnazoziomba, dua na Mioyo yenu misafi ndio maendeleo ya kitu hichi kizuri,” aliongezea Sheikh Mustapha.

“Kuna viongozi sio Waislamu lakini wameshiriki katika ujenzi wa misikiti mbalimbali iliyopo hapa nchini.

“Kwahiyo niwaombe viongozi na walimu kuacha kubeba maneno ya uchonganishi yasiyoleta maendeleo na inatubidi tuyakemee,” alisema Sheikh Mustafa.

Sanjari na hayo Sheikh Mustapha aliweza kutoa michango katika kusaidia ujenzi wa Madrasa na  Misikiti inayoendelea kujengwa ikiwa ni moja ya kuweka hamasa kwa watu kuchangia na Swawabu kwa Allah S.W.A

About the author

mzalendoeditor