Muonekano wa Bandari ya Dar es Salaam… |
Muonekano wa Bandari ya Dar es Salaam… |
*Meli kubwa ya MERIDIAN ACE
MELI kubwa ya shehena ya magari inatarajia kuwasili kwenye bandari ya Dar es Salaam. Meli hiyo kutoka Japan na Singapore itawasili Dar es Salaam Mei 9, 2022 ikiwa na magari 4397 idadi ambayo haijawahi kufikiwa kwa pamoja. Hii ndio rekodi kubwa kuliko zote. Rekodi ya mwisho ilikuwa magari 4041 yaliyowasili Aprili 08 2022.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA Bw. Nicodemus Mushi imesema, mafanikio hayo ni matokeo ya kazi kubwa ya kutangaza Uwezo wa Bandari za Tanzania, inayofanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Awamu ya Sita kote ulimwenguni.
Amesema uwekezaji mkubwa umefanywa na Serikali katika Vitendea kazi na Maboresho ya Miundombinu ya kibandari sambamba na Kampeni za Kimasoko na ushirikiano thabiti wa TPA, wateja na wadau wake wengine.