Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Filamu ya The Royal Tour leo Mei 8, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC). Pamoja naye ni Viongozi mbalimbali wa Kitaifa wakiwemo Rais wa Zanzibar, Mhe. Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson na Viongozi wengine.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakifatilia Uzinduzi wa Tanzania The Royal Tour ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Viongozi mbalimbali wakifatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Kitaifa wa Filamu ya The Royal Tour leo Mei 8, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC). Pamoja naye ni Viongozi mbalimbali wa Kitaifa wakiwemo Rais wa Zanzibar, Mhe. Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson na Viongozi wengine.