Featured Kitaifa

MAZUNGUMZO YA FAMILIA YANACHANGIA KUONDOKANA NA MASUALA YA UKATILI

Written by mzalendoeditor

 Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akiwasili katika soko la Mbezi Luis leo Mei 7,2022 na kuongea na baadhi ya wananchi wa aneo hilo kuelekea Siku ya Kimataifa ya Familia (Mei 15) ambayo hudhimishwa na nchi zilizo Wanachama wa Umoja wa Mataifa.  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na mmoja wa wafanyabiashara wa soko la Mbezi Luis leo Mei 7,2022 Siku ya Kimataifa ya Familia (Mei 15) ambayo hudhimishwa na nchi zilizo Wanachama wa Umoja wa Mataifa  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wafanyabiashara wa mbogamboga katika soko la Mbezi Luis leo Mei 7,2022 Jijini Dar es Salaam kuelekea Siku ya Kimataifa ya Familia (Mei 15) ambayo hudhimishwa na nchi zilizo Wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa Tamko Namba 47/237 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la tarehe 20 Septemba, 1993.  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wananchi wa Soko la Mbezi Luis kuelekea Siku ya Kimataifa ya Familia (Mei 15) ambayo hudhimishwa na nchi zilizo Wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa Tamko Namba 47/237 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la tarehe 20 Septemba, 1993.  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi wa soko la Mbezi Luis kuhusu kuelekea Siku ya Kimataifa ya Familia (Mei 15) ambayo hudhimishwa na nchi zilizo Wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa Tamko Namba 47/237 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la tarehe 20 Septemba, 1993.   Baadhi ya wananchi wa soko la Mbezi Luis wakimsikiliza Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza kwenye na wananchi wa soko hilo.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema mazungumzo ya familia yanasaidia kuimarisha ulinzi kwa mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili ambavyo vinaendelea kuongezeka nchini.

Ameyasema hayo leo Mei 7,2022 wakati alipofanya ziara katika Soko la Mbezi Luis Jijini Dar es salaam na kuzungumza na wananchi katika kuelekea Siku ya Kimataifa ya Familia (Mei 15) ambayo hudhimishwa na nchi zilizo Wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa Tamko Namba 47/237 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la tarehe 20 Septemba, 1993. 

Akizungumza na wananchi katika eneo hilo Waziri Gwajima amesema Mazungumzo ya Familia yakifanyika kwa weledi yana tija kubwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa familia na maendeleo ya mtoto katika nyanja za elimu, lishe, afya, maadili na utamaduni. 

“Mazungumzo ya familia yanaimarisha mahusiano na ushirikiano katika familia na hivyo kupunguza athari za migogoro ya ndoa ambayo kwa kiasi kikubwa inakwamisha maendeleo ya familia”. Amesema 

Aidha Waziri Gwajima amesema kwa kuwa na siku hii ya Mazungumzo ya Familia itawakumbusha wadau umuhimu wa familia na bila shaka itasaidia kujenga utamaduni wa wanafamilia kukutana na kujadiliana juu ya masuala yanayowahusu bila shinikizo kutoka nje ya familia.

Kwa upande wa wananchi wamechangia mawazo yao huku wengi wao wakisema tatizo la kuharibika kwa mtoto kitabia hutokana na malezi ya wazazi wao.

Bw.Samweli Muhonge ambaye ni Mwalimu wa Elimu Jumuishi kwa watoto wenye usonji na upofu, amesema changamoto ambayo ipo kwasasa hivi tumeacha malezi jumuishi ya jamii na kuwaachia familia husika, pale mtoto anapofanya tukio au jambo linalokwenda kinyume na maadili asisubiriwe mama au baba wa mtoto huyo mpaka yeye kuchukua hatua.

“Wazazi mara nyingi tumekuwa tupo kwenye mihangaiko ya kila siku kwahiyo ni jukumu la jamii nzima kuona kila mmoja anachangia kumjenga mtoto ambaye kesho ni kiongozi na tunnapokaa kimya, dosali yoyote itakayopatikana sio kosa la baba wala mama ni la jamii nzima”. Amesema 

Nae Bi.Mwajuma Mohamed amesema malezi bora yanaondoka kutokana na wazazi kuacha malezi bora ya zamani kwani mtoto akifanya kosa kuna ulazimu wa mtu yoyote kutoa adhabu asisubiriwe mzazi wake ndie atoe adhabu.

About the author

mzalendoeditor