Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akitoa salamu za rambirambi za serikali wakati wa ibada ya mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Ziwa Tanganyika la Kanisa la Moravian,Askofu Charles Katale mazishi yaliofanyika katika eneo la Kanisa la Moravian Mwanga mkoani Kigoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Ziwa Tanganyika la Kanisa la Moravian,Askofu Charles Katale wakati wa ibada ya mazishi yaliofanyika katika eneo la Kanisa la Moravian Mwanga mkoani Kigoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Ziwa Tanganyika la Kanisa la Moravian,Askofu Charles Katale wakati wa mazishi yaliofanyika katika eneo la Kanisa la Moravian Mwanga mkoani Kigoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Ziwa Tanganyika la Kanisa la Moravian,Askofu Charles Katale wakati wa mazishi yaliofanyika katika eneo la Kanisa la Moravian Mwanga mkoani Kigoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwafariji wanafamilia wa aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Ziwa Tanganyika la Kanisa la Moravian,Askofu Charles Katale mara baada ya mazishi ya Askofu huyo yaliofanyika katika eneo la Kanisa la Moravian Mwanga mkoani Kigoma.
…………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 07 Mei 2022 amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Ziwa Tanganyika la Kanisa la Moravian Tanzania ,Askofu Charles Katale, mazishi yaliofanyika katika eneo la kanisa la Moravian Mwanga mkoani Kigoma.
Akitoa salamu za rambirambi za serikali, Makamu wa Rais amesema serikali imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha askofu Katale na kuwapa pole familia, kanisa na watanzania kwa ujumla kwa kumpoteza kiongozi huyo ambaye aliishi vema wito wake wa kiuchungaji.
Amesema serikali inatambua mchango wa Askofu Katale na kanisa la Moravian kwa ujumla kwa mafundisho wanayotoa kwa watanzania kimwili na kiroho na kuwaombea heri katika kumpata kiongozi wa jimbo hilo la ziwa Tanganyika atakaendeleza kazi alioianza marehemu Askofu Katale.
Aidha Makamu wa Rais amewaomba viongozi wa dini zote nchini kuendelea kuwakumbusha waumini wajibu walionao katika jamii ikiwemo kuwajibika kuwasaidia wale wasiojiweza wakiwemo yatima na wajane. Pia amewasihi kuwafundisha waumini juu ya upendo baina yao ili kuwa na Tanzania yenye amani na utulivu.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amewapongeza kanisa la Moravian Tanzania kwa kuitikia wito wa serikali wa kuhamasisha wananchi kujitokeza katika zoezi la sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Kwa upande wake Askofu Kiongozi Conrad Nguvumali ameishukuru serikali kwa faraja waliotoa kwa kanisa katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na kiongozi wa kanisa hilo. Aidha amesema kanisa la Moravian litaendelea kushirikiana na serikali katika kuhamasisha waumini kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi ili kuisaidia serikali kupanga vema mipango yake.