Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohamed Khamis Abdulla (mwenye suti) akikagua kibao cha Anwani ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa zoezi la Anwani za Makazi katika mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohamed Khamis Abdulla (mwenye suti) akikagua namba ya nyumba katika eneo la Mji Mkongwe zilizowekwa enzi za ukoloni wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa zoezi la Anwani za Makazi katika mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohamed Khamis Abdulla (mwenye suti) akikagua mchoro unaoonesha uwekaji wa miundombinu ya Anwani za Makazi katika mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohamed Khamis Abdulla (wa kwanza kulia) akiwa akipita katika barabara na mitaa ya mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar kukagua uwekaji wa miundombinu ya Anwani za Makazi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohamed Khamis Abdulla (kulia) azungumza na Katibu Tawala wa mkoa wa Mjini Magharibi, Bi Radhiya Rashid Haroub wakati wa kikao chake na watendaji wa mkoa huo cha kupokea utekelezaji wa zoezi la Anwani za Makazi katika mkoa huo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohamed Khamis Abdulla (mwenye suti) akikagua marumaru yenye jina la mtaa wa Kibokoni uliopo katika Mamlaka ya Mji Mkongwe mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.
…………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla ameainisha faida za Anwani za Makazi pamoja na zoezi la sensa ya watu na makazi kuwa ni pamoja na kurahisisha ufikishaji wa huduma za kijamii na kiuchumi mathalani majanga ya njaa na mafuriko iwapo yakitokea Serikali itahitaji kutambua idadi ya watu ili kuwafikishia huduma kulingana na uhitaji
Akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua na kuhamasisha utekelezaji wa operesheni ya Anwani za Makazi katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Bwana Abdulla amesisitiza watendaji kuongeza kasi ya utekelezaji wa operesheni ya Anwani za Makazi ili kukamilisha kwa muda uliopangwa na Serikali
Amesema kuwa zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika Agosti mwaka huu linategemea Mfumo wa Anwani za Makazi ili kuwarahisishia wale watakaofanyakazi ya kuhesabu watu kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kwa kuwa sensa ya mwaka huu itafanyika kidijitali kupitia mfumo huo wa utambuzi wa wakazi na makazi
Katika ziara hiyo, Bwana Abdulla amefanikiwa kutembelea na kuona baadhi ya majina ya mitaa yaliyowekwa kwa marumaru “marbles” na namba za nyumba zilizokuwepo toka enzi za mkoloni katika mitaa ya Mji Mkongwe uliopo katika mkoa huo ambazo zitaendelea kutumika na tayari zimeshaingizwa kwenye mfumo wa utambuzi wa NaPA
Aidha, nguzo zenye majina ya barabara zitawekwa kwenye barabara 11 za makutano katika maeneo mbalimbali ya Mamlaka ya Mji Mkongwe na marumaru 180 zenye majina ya mitaa zitawekwa kwenye mitaa ambayo haina ili kukamilisha zoezi la uwekaji wa miundombinu hiyo
Kama tunavyofahamu, Februari 8, mwaka huu wa 2022, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alitangaza utekelezaji wa mfumo wa Anwani za Makazi kuwa operesheni maalumu kwa gharama ya jumla ya shilingi bilioni 28 kwenye mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inaendelea kukagua, kuhamasisha, kusimamia na kusaidia utekelezaji wa operesheni ya Anwani za Makazi kupitia wataalamu waratibu waliopelekwa katika kila mkoa pamoja na ziara zinazofanywa na viongozi wa Wizara hiyo ili kuhakikisha kila mkoa unafikia lengo na matarajio ya Serikali ya kukamilisha kabla ya Mei 22 mwaka huu