Featured Kitaifa

WAZIRI MKENDA ATETA NA MKUU WA IDARA YA ELIMU UNICEF DKT.DANIEL BAHETA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (kulia) akizungumza na Mkuu wa Idara ya Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) ofisi ya Tanzania Dkt. Daniel Buheti (Kushoto). Dkt.Baheta alimtembelea Waziri Mkenda ofisini kwake jijini Dodoma kujadiliana mambo mbalimbali yahusuyo mageuzi ya elimu nchini.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (katikati) akizungumza na Mkuu wa Idara ya Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto (UNICEF) ofisi ya Tanzania Dkt. Daniel Baheta (Kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Sekta ya Elimu UNESCO Tanzania Faith Shayo walipokutana katika ofisi za Wizara jijini Dodoma kujadiliana mambo mbalimbali kuhusu mageuzi ya elimu nchini.Picha na Wizara ya Elimu

…………………………………..

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (Mb) leo Mei 6, Jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Idara ya Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto Ofisi ya Tanzania (UNICEF) Dkt. Daniel Baheta na Mkuu wa Sekta ya Elimu UNESCO kwa upande wa Tanzania Faith Shayo kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu elimu kuelekea Mkutano wa Kimataifa wa Elimu utakaofanyika mwezi Septemba 2022 nchini Marekani wenye lengo la kuleta mabadiliko Chanya katika Sekta ya Elimu.

Katika kikao hicho Waziri Mkenda aliwahakikishia mashirika hayo ushirikiano katika kuleta mageuzi ya elimu nchini.

About the author

mzalendoeditor