Featured Kitaifa

BASHUNGWA AFANYA MABADILIKO YA WATUNZA FEDHA

Written by mzalendoeditor

WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Mei 5,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu mapato na matumizi ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Machi 2022 (Robo ya tatu ya mwaka wa Fedha 2021/22)

……………………………………………………………………………………………

WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa, amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Vitengo vya Fedha wa Halmashauri (Wekahazina).

Waziri Bashungwa ameyasema hayo leo Mei 05, 2022 Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya mapato na matumizi ya Halmashauri kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa Fedha 2021/22.

Waziri Bashungwa amesema kuwa wameshawabadilishia vituo Wakuu wa Vitengo hivyo 109, kuwabadilishi majukumu Wakuu wa Vitengo vya Fedha 16 huku 72 wakiendelea kubaki kwenye Vituo vyao vya awali na 3 wakiwa kwenye matazamio.

‘Nitaendelea kufanya mabadiliko kila wakati inapobidi. Katika eneo hili napenda kutoa salamu kwa Wakurugenzi na Wakuu wa Kitengo cha Fedha kuwa, sitavumilia kabisa uzembe katika ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya Serikali ”amesema Waziri Bashungwa 

About the author

mzalendoeditor