NA MWANDISHI WETU, TANGA.
MAAFISA wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Makao Makuu pamoja na Bandari ya Tanga wamefanya ziara ya kuwatembea wadau wa kanda ya Kaskazini.
Lengo la ziara hiyo ya wadau wa kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Arusha ambapo nia ya ziara hiyo ni kuongea na wateja wao ili kuweza kujua changamoto mbalimbali wanazozipata pindi wanapotumia bandari.
Licha ya hivyo pia pamoja na kuwatangazia huduma zinazotarajiwa kutolewa katika Bandari ya Tanga baada ya maboresho makubwa yaliyofanywa.
Hata hivyo wameipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu kwa maboresho makubwa yanayoendelea katika Bandari Kongwe ya Tanga.