Featured Kitaifa

WAZIRI MCHENGERWA,DKT ABBASI WASHIRIKI SWALA YA EID EL FITRI

Written by mzalendoeditor

Na. John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed
Mchengerwa  na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Dkt. Hassan Abbasi leo Mei 3,
2022 wameungana  na Viongozi Wakuu wa Nchi na waumini wa dini ya
Kiislamu kushiriki Swala ya Eid El Fitri iliyofanyika kitaifa katika
Msikiti Mkuu wa BAKWATA Kinondoni Muslim Jijini Dar es Salaam.

Swala hiyo  imeongozwa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania,
Abubakar Zubeir na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu. Mhe, Kassim Majaliwa
Majaliwa.

Katika Swala hiyo, Mufti wa Tanzania  ametoa wito kwa
waislam wote nchini kujitokeza na kushiriki kikamifu zoezi la kitaifa la
Sensa  litakalofanyika Agosti 23 mwaka huu nchini.

Mufti Zubeir  amefafanua kwamba muislam kukataa kuhesabiwa
kwa kigezo kuwa kitendo cha kuhesabiwa ni haramu siyo msingi wa dini ya
kiislam na kuwataka kushiriki kikamilifu zoezi hilo kwa maendeleo ya
taifa letu kwa ujumla.

Sensa ni zoezi muhimu kwa taifa lolote duniani kwa kuwa linasaidia Serikali kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo kwa ufanisi.

About the author

mzalendoeditor