Featured Kitaifa

RAIS DK.MWINYI AJUMUIKA NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM KATIKA SALA YA EID ELFITY MASJID JAMIU ZINJIBAR MAZIZINI ZANZIBAR

Written by mzalendoeditor

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Serikali na Dini baada ya kuwasili katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja kuhudhuria Sala ya Eid Fitry baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Sala hiyo iliyofanyika katika Masjid hiyo leo 3-4-2022.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika Sala ya Eid Fitry iliyofanyika leo asubuhi katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja Jijini Zanzibar, baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utwala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Mohammed Gharib Bilal na  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika viwanja vya Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Unguja wakati ikipingwa mizinga baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid Fitry iliyofanyika katika Masjid hiyo na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.(Picha na Ikulu)

About the author

mzalendoeditor