Featured Kitaifa

WAZIRI NAPE NNAUYE ATEMBELEA BANDA LA STAMICO MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI JIJINI ARUSHA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) akiwa katika Banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Madini Mchenjuaji wa Shirika la STAMICO Happy Mbenyange kuhusu shughuli wanazofanya leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha. Waziri Nape Nnauye ametembelea banda la STAMICO wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti’. Picha na Kadama Malunde 1 blog 
Mhandisi wa Madini Mchenjuaji wa Shirika la STAMICO Happy Mbenyange akimwelezea Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) kuhusu Mkaa Mbadala uliopewa jina la Rafiki Briquettes unaotengenezwa kutokana na makaa ya mawe kutoka Mgodi wa Makaa ya Mawe STAMICO Kiwira – Kabulo mkoani Mbeya.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akiipongeza STAMICO kwa shughuli wanazofanya alipotembelea banda la STAMICO wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani Jijini Arusha yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti’. Kulia ni Mhandisi wa Madini Mchenjuaji wa Shirika la STAMICO Happy Mbenyange
 
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

About the author

mzalendoeditor