Na Mwandishi Wetu,ARUSHA
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka wafungwa wanaopata msamaha wa Rais wa vifungo kutoka gerezani kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi kwa kutojihusisha tena kwenye makosa ya uvunjifu wa sheria na kuwa kero kwa wananchi kwa kufanya vitendo vya kihalifu.
IGP Sirro amesema hayo akiwa jijini Arusha wakati akizungumza na Maofisa waandamiziwa wa Jeshi hilo.
Kuhusu ajali za barabarani IGP Sirro amewataka madereva wa pikipiki maarufu bodaboda kufuata sheria za usalama barabarani ikiwa pamoja na kuva kofia ngumu huku akiwaonya baadhi ya wananchi kuacha kujiingiza kwenye uhalifu wa mifugo pamoja na uhalifu wa kutumia silaha za moto na kwamba mwananchi yeyote atakayefanikisha kutoa taarifa na kukamatwa kwa mtuhumiwa wa aina hiyo atazawadiwa kiasi cha shilingi milioni moja.
Akizungumzia suala la mashine ya kielektroniki kwa ajili ya kukusanya maduhuli ya serikali IGP Sirro amewataka watumia wa vyombo vya moto kutii sheria bila shuruti.