Featured Michezo

YANGA YATUMA SALAMU KWA SIMBA,YAVUNJA MWIKO KWA NAMUNGO

Written by mzalendoeditor

Mabingwa wa kihistoria timu ya Yanga imetuma salamu kwa watani zao Simba kuelekea katika mechi yao itakayopigwa April 30 mwaka huu baada ya kuitandika  na Kuvunja mwiko didi ya Namungo FC kwa kupata ushindi wa   mabao 2-1 mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao hatari Fiston Mayele dakika ya 17 akipiga tobo mlinda mlango David Mapigano.

Shiza Kichuya aliisawazishia Namungo dakika ya 33 akifunga bao safi kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Yanga Diarra Djigui bao la ushindi kwa Yanga limewekwa kimiani na Feisal Salum ‘Fei Toto’ dakika ya 38.

Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 54 na kuendelea kujichimbia kilele mwa msimamo wa Ligi hiyo huku wakituma salamu wa watani zao Simba ambao mechi yao dhidi ya watani utapigwa April 30,2022.

About the author

mzalendoeditor