Mkuu wa Kitengo cha ufuatiliaji wa tathmini ya udhibiti wa Malaria, Dk.Sijenunu Aron akitoa mada ya hali ya Maralia nchini katika semina ya waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya Malaria ambapo hufanyika kila Aprili 25 kila mwaka duniani iliyofanyika leo April 20,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha udhibiti wa Mbu waenezao Malaria Bw.Winfred Mwafongo,akielezea mkakati wa udhibiti wa Mbu waenezao Malaria kwa njia ya utangamano wakati wa semina ya waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya Malaria ambapo hufanyika kila Aprili 25 kila mwaka duniani iliyofanyika leo April 20,2022 jijini Dodoma.
Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria Dk.Abdallah Lusasi akitoa mada kuhusu mkakati wa uchunguzi,Matibabu wa Malaria na Tiba Kinga kwa wajawazito wakati wa semina ya waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya Malaria ambapo hufanyika kila Aprili 25 kila mwaka duniani iliyofanyika leo April 20,2022 jijini Dodoma.
Afisa wa Kitengo cha uhamasishaji na uraghabishi kuhusu udhibiti wa Malaria Theresia Shirima,wakati wa semina ya waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya Malaria ambapo hufanyika kila Aprili 25 kila mwaka duniani iliyofanyika leo April 20,2022 jijini Dodoma.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Afya Catherine Sungura,akizungumza wakati wa semina ya waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya Malaria ambapo hufanyika kila Aprili 25 kila mwaka duniani iliyofanyika leo April 20,2022 jijini Dodoma.
Mwandishi wa habari kutoka Chanel ten Kuringe Mongi,akiuliza swali wakati wa semina ya waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya Malaria ambapo hufanyika kila Aprili 25 kila mwaka duniani iliyofanyika leo April 20,2022 jijini Dodoma.
Mwandishi wa habari kutoka Uhuru Selina Mathew akiuliza swali wakati wa semina ya waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya Malaria ambapo hufanyika kila Aprili 25 kila mwaka duniani iliyofanyika leo April 20,2022 jijini Dodoma.
Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mkoa wa Dodoma wakifatilia mada mbalimbali wakati wa semina ya waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya Malaria ambapo hufanyika kila Aprili 25 kila mwaka duniani iliyofanyika leo April 20,2022 jijini Dodoma.
………………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
IMEELEZWA kuwa kutokana na utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa vifo vitokanavyo na ugonjwa wa Malaria nchini vimepungua kwa asilimia 70.
Hayo yameelezwa leo April 20,2022 jijinni Dodoma na Mkuu wa Kitengo cha ufuatiliaji wa tathmini ya udhibiti wa Malaria, Dk.Sijenunu Aron,wakati akitoa mada ya hali ya Maralia nchini katika semina ya waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya Malaria ambapo hufanyika kila Aprili 25 kila mwaka duniani.
Amesema kuwa utafiti unaonesha kuwa maambukizi kwa watoto wa shule za msingi yamepungua kutoka asilimia 21.6 mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 11.2 mwaka 2021.
Dk. Aron amesema kuwa idadi ya wagonjwa imepunguwa kwa asilimia 53 kwa kila wagonjwa 1000 kutoka wagonjwa 162 hadi kufikia wagonjwa 76.
”Wagonjwa waliolazwa kutokana na Malaria imepungua kwa asilimia 32 kutoka wagonjwa 307,88 mwaka 2017 hadi 209,888 mwaka 2021 wakati vifo vimepungua kwa asilimia 70 kati ya vifo 100,000 kutoka vifo 6,311 mwaka 2015 hadi 1,909 mwaka 2021”amesema Dk.Aron
Dk. Aron amesema kuwa pamoja na kupunguwa kwa Malaria hadi kufikia asilimia 7.5 mwaka 2017, bado aslimia 94 ya watanzania wako katika hatari ya kupata maambukizi ya uongojwa huo.
Hata hivyo amesema kuwa mikoa ambayo ina kiwango kikubwa cha Malaria ni Lindi, Mtwara, Pwani, Ruvuma, Tanga na Tabora wakati ile yenye kiwango kidogo ni Kilimanjaro, Manyara, Arusha, Dodoma, Iringa, Singida na Njombe.
Dk.Aron amesema kuwa takwimu za dunia za mwaka 2021, zinaonesha kuwa kwa mwaka 2020 kulikuwa na ongezeko la wagonjwa wanaokadiriwa kufikia milioni 241 katika nchi 85 zenye ugonjwa huo kutoka wagonjwa milioni 227 huku vifo vikiongezeka hadi kufikia vifo 627,000 kukiwa na ongezeko la vifo 69,000 sawa na asilimia 12 ikilinganishwa na vifo 558,000 kwa mwaka 2019 .
Kwa upande wake Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria kutoka Wizara ya afya Dk.Abdallah Lusasi ,amesema kuwa hali ya malaria nchini kwa sasa imepungua sana mwaka 2017 tafiti zilionyesha kuwa tulikuwa na malaria asilimia 7.5 lakini sisi tuna mpango mkakati wa kuhakikisha 2023 tunafikia asilimia 5,Mwaka 2025 tufikie asilimia 3.5 na mwaka 2030 tunatokomeza malaria kabisa nchi nzima.