Featured Michezo

HAALAND MBIONI KUJIUNGA NA MANCHESTER CITY

Written by mzalendoeditor

TIMU ya Manchester City imepiga hatua kubwa katika kumsajili Mshambuliaji Erling Haaland (21) baada ya klabu hiyo kukubaliana na wawakilishi wa mchezaji huyo.

Inaelezwa kuwa fungu kubwa la fedha litakalomfanya Haaland kuwa mchezaji anayelipwa zaidi ya Pauni 500,000 kwa wiki kwenye Ligi Kuu ya England limeandaliwa na Man. City

Man. City inatarajiwa kulipa Paundi Milioni 63 kwa klabu ya Borussia Dortmund ili kumnasa Haaland, ikiwa yote yataenda kulingana na mpango, inadaiwa mchezaji huyo atapewa mkataba wa miaka mitano na usajili unaweza kukamilika wiki ijayo

About the author

mzalendoeditor