Featured Kitaifa

BIBI MATATANI KWA TUHUMA ZA KUUA MJUKUU WAKE

Written by mzalendoeditor

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mwanamke Tatu Moshi Misungwi mwenye miaka 45 mkazi wa Kijiji na Kata ya lyabukande w Halmashairi ya Shinyanga kwa kuwapiga wajukuu zake wawili na kuwamwagia maji ya moto hali iliyopelekea mtoto mmoja kufariki mapema jana, Jumatatu Aprili 18.

Kamanda wa Polisi wa mkoani Shinyanga, ACP George Kyando amemtaja marehemu kuwa ni Joseph Juma aliyekuwa na miaka minne na majeruhi ni Limi Lameck Matihas aliyekuwa na mwaka mmoja na miezi saba (7).

Kamanda Kyando amesema kuwa jeshi hilo pia linamshikiria mama wa watoto hao aitwaye Hellen Nicolaus kwa kushindwa kutoa taarifa kwa viongozi wa kijiji au eneo hilo na kuendelea kushuhudia bibi yao akifanya vitendo hivyo vya kikatili kwa watoto wake.

ACP Kyando amebainisha kuwa mara baada ya uchunguzi kukamilka watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakili ikiwemo kujeruhi na kusababisha kifo.

CHANZO:AZAM TV

About the author

mzalendoeditor